Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 9:6-14 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 9:6-14 in Biblia Takatifu

6 Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni,
7 akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Basi, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
8 Basi, jirani zake na wale waliokuwa wanajua kwamba hapo awali alikuwa maskini mwombaji, wakasema, “Je, huyu siye yule maskini aliyekuwa akiketi na kuomba?”
9 Baadhi yao wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “La! Ila anafanana naye.” Lakini huyo aliyekuwa kipofu akasema, “Ni mimi!”
10 Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?”
11 Naye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka machoni na kuniambia: Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu. Basi, mimi nikaenda, nikanawa, nikapata kuona.”
12 Wakamwuliza, “Yeye yuko wapi?” Naye akawajibu, “Mimi sijui!”
13 Kisha wakampeleka huyo mtu aliyekuwa kipofu kwa Mafarisayo.
14 Siku hiyo Yesu alipofanya tope na kumfumbua macho mtu huyo, ilikuwa siku ya Sabato.
Yohana 9 in Biblia Takatifu

Yohana 9:6-14 in Biblia ya Kiswahili

6 Baada ya Yesu kusema maneno haya, alitema kwenye ardhi, alifanya tope kwa mate, na akampaka yule mtu machoni na lile tope.
7 Akamwambia, nenda kaoge katika kisima cha Siloam (Inayotafsiriwa kama 'aliyetumwa').” Kwa hiyo huyo mtu alienda, akanawa, na akarudi, anaona.
8 Majirani wa yule mtu na wale waliomuona mwanzo kama mwombaji walisema, Je! huyu siye yule mtu aliyekuwa akikaa na kuomba?” wengine walisema, “Ni yeye.”
9 Na wengine walisema, “Hapana, bali anafanana naye.” Lakini alikuwa akisema, “Ni mimi.”
10 Wakamwambia, “Sasa macho yako yalifunguliwaje?”
11 Alijibu, mtu aitwaye Yesu alifanya tope na kupaka macho yangu na kuniambia, 'Nenda Siloam ukanawe.' Kwa hiyo nilienda, na nikanawa, na nikapata kuona tena.”
12 Wakamwambia, “Yuko wapi?” Alijibu, “Sijui.”
13 Wakampeleka yule mtu aliyewahi kuwa kipofu kwa Mafarisayo.
14 Nayo ilikuwa siku ya Sabato wakati Yesu alipotengeneza tope na kuyafumbua macho yake.
Yohana 9 in Biblia ya Kiswahili