Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 9:34-41 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 9:34-41 in Biblia Takatifu

34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuzia mbali.
35 Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuzia mbali, naye alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
36 Huyo mtu akajibu, “Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipate kumwamini.”
37 Yesu akamwambia, “Umekwisha mwona, naye ndiye anayesema nawe sasa.”
38 Basi, huyo mtu akasema, “Ninaamini Bwana!” Akamsujudia.
39 Yesu akasema, “Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu, kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawe vipofu.”
40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye walisikia maneno hayo, wakamwuliza, “Je, sisi pia ni vipofu?”
41 Yesu akawajibu, “Kama mngekuwa vipofu, hamngekuwa na hatia; lakini sasa ninyi mwasema: Sisi tunaona, na hiyo yaonyesha kwamba mna hatia bado.
Yohana 9 in Biblia Takatifu

Yohana 9:34-41 in Biblia ya Kiswahili

34 Walijibu na kumwambia, “Ulizaliwa katika dhambi kabisa, na wewe unatufundisha sisi?” Ndipo walipomfukuza kutoka katika sinagogi.
35 Yesu alisikia kwamba wamemwondoa kwenye sinagogi. Alimpata na kumwambia, “Unamwamini Mwana wa Mtu?”
36 Alijibu na kusema, “Ni nani, Bwana, ili nami nipate kumwamini?”
37 Yesu akamwambia, “Umeshamuona, naye unayezungumza naye ndiye.”
38 Yule mtu akasema, “Bwana, Naamini.” Ndipo akamsujudia.
39 Yesu akasema, “Kwa hukumu nimekuja katika Ulimwengu huu ili kwamba wale wasioona wapate kuona na wale wanaoona wawe vipofu.”
40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye wakasikia maneno hayo na kumwuliza, “Na sisi pia ni vipofu?”
41 Yesu akawaambia, “Kama mngelikuwa vipofu, msingelikuwa na dhambi. Hata hivyo, sasa mnasema, 'Tunaona,' dhambi yenu inakaa.”
Yohana 9 in Biblia ya Kiswahili