Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 9:29-37 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 9:29-37 in Biblia Takatifu

29 Sisi tunajua kwamba Mungu alisema na Mose, lakini mtu huyu hatujui ametoka wapi!”
30 Naye akawajibu, “Hili ni jambo la kushangaza! Ninyi hamjui ametoka wapi, lakini amenifumbua macho yangu!
31 Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake.
32 Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
33 Kama mtu huyu hakutoka kwa Mungu, hangeweza kufanya chochote!”
34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuzia mbali.
35 Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuzia mbali, naye alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
36 Huyo mtu akajibu, “Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipate kumwamini.”
37 Yesu akamwambia, “Umekwisha mwona, naye ndiye anayesema nawe sasa.”
Yohana 9 in Biblia Takatifu

Yohana 9:29-37 in Biblia ya Kiswahili

29 Tunajua kwamba Mungu alizungumza na Musa, lakini kwa huyu mtu, hatujui kule atokako.”
30 Yule mtu akajibu na kuwaambia, “Kwa nini, hili ni jambo la kushangaza, kwamba hamjui anakotoka, na bado ameyafumbua macho yangu.
31 Tunajua kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini ikiwa mtu yeyote anamwabudu Mungu na hufanya mapenzi yake, Mungu humsikiliza.
32 Tangu kuanza kwa Ulimwengu haijawahi kamwe kusikiwa kwamba yeyote ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
33 Ikiwa mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingelifanya chochote.”
34 Walijibu na kumwambia, “Ulizaliwa katika dhambi kabisa, na wewe unatufundisha sisi?” Ndipo walipomfukuza kutoka katika sinagogi.
35 Yesu alisikia kwamba wamemwondoa kwenye sinagogi. Alimpata na kumwambia, “Unamwamini Mwana wa Mtu?”
36 Alijibu na kusema, “Ni nani, Bwana, ili nami nipate kumwamini?”
37 Yesu akamwambia, “Umeshamuona, naye unayezungumza naye ndiye.”
Yohana 9 in Biblia ya Kiswahili