Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 7:2-12 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 7:2-12 in Biblia Takatifu

2 Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
3 Basi ndugu zake wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.
4 Mtu hafanyi mambo kwa siri kama anataka kujulikana kwa watu. Maadam unafanya mambo haya, basi, jidhihirishe kwa ulimwengu.”
5 (Hata ndugu zake hawakumwamini!)
6 Basi, Yesu akawaambia, “Wakati wangu ufaao haujafika bado. Lakini kwenu ninyi kila wakati unafaa.
7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini mimi wanichukia kwa sababu mimi nauambia wazi kwamba matendo yake ni maovu.
8 Ninyi nendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo, maana saa yangu ifaayo haijafika.”
9 Alisema hayo kisha akabaki huko Galilaya.
10 Baada ya ndugu zake kwenda kwenye sikukuu, Yesu naye alikwenda, lakini hakuenda kwa hadhara bali kwa siri.
11 Viongozi wa Wayahudi walikuwa wanamtafuta kwenye sikukuu hiyo; Wakauliza: “Yuko wapi?”
12 Kulikuwa na minong'ono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”
Yohana 7 in Biblia Takatifu

Yohana 7:2-12 in Biblia ya Kiswahili

2 Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
3 Ndipo ndugu zake walipomwambia, “Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.
4 Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu.”
5 Hata ndugu zake pia hawakumwamini.
6 Ndipo Yesu alipowaambia, “Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.
7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.
8 Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado.”
9 Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.
10 Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.
11 Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, “Yuko wapi?”
12 Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “Hapana, huwapotosha makutano.”
Yohana 7 in Biblia ya Kiswahili