Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 6:68-71 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 6:68-71 in Biblia Takatifu

68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tutakwenda kwa nani? Wewe unayo maneno yaletayo uzima wa milele.
69 Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu.”
70 Yesu akawaambia, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Hata hivyo, mmoja wenu ni Ibilisi!”
71 Yesu alisema hayo juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti; maana huyu alikuwa ndiye atakayemsaliti, ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili.
Yohana 6 in Biblia Takatifu

Yohana 6:68-71 in Biblia ya Kiswahili

68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele,
69 na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu.”
70 Yesu akawambia, “Je mimi sikuwachagua ninyi, na mmoja wenu ni ibilisi?
71 Sasa alikuwa akiongea kuhusu Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, kwa kuwa alikuwa ni yeye akiwa mmoja wa wale kumi na wawili, ambaye ndiye angemsaliti Yesu.
Yohana 6 in Biblia ya Kiswahili