Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 6:54-70 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 6:54-70 in Biblia Takatifu

54 Anayekula mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele nami nitamfufua siku ya mwisho.
55 Maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, akaa ndani yangu, nami nakaa ndani yake.
57 Baba aliye hai alinituma, nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye mimi ataishi pia kwa sababu yangu.
58 Basi, huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokula babu zetu, wakafa. Aulaye mkate huu ataishi milele.”
59 Yesu alisema hayo alipokuwa akifundisha katika sunagogi kule Kafarnaumu.
60 Basi, wengi wa wafuasi wake waliposikia hayo, wakasema, “Haya ni mambo magumu! Nani awezaye kuyasikiliza?”
61 Yesu alijua bila kuambiwa na mtu kwamba wanafunzi wake walikuwa wananung'unika juu ya jambo hilo, akawauliza, “Je, jambo hili linawafanya muwe na mashaka?
62 Itakuwaje basi, mtakapomwona Mwana wa Mtu akipanda kwenda kule alikokuwa kwanza?
63 Roho ndiye atiaye uzima; binadamu peke yake hawezi. Maneno niliyowaambieni ni Roho, ni uzima.
64 Hata hivyo, wako baadhi yenu wasioamini.” (Yesu alisema hivyo kwani alijua tangu mwanzo ni kina nani wasioamini, na pia ni nani atakayemsaliti.)
65 Kisha akasema, “Ndiyo maana niliwaambieni kwamba hakuna awezaye kuja kwangu asipowezeshwa na Baba yangu.”
66 Kutokana na hayo, wengi wa wafuasi wake walirudi nyuma wasiandamane naye tena.
67 Basi, Yesu akawauliza wale kumi na wawili, “Je, nanyi pia mwataka kwenda zenu?”
68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tutakwenda kwa nani? Wewe unayo maneno yaletayo uzima wa milele.
69 Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu.”
70 Yesu akawaambia, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Hata hivyo, mmoja wenu ni Ibilisi!”
Yohana 6 in Biblia Takatifu

Yohana 6:54-70 in Biblia ya Kiswahili

54 Yeyote aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.
55 Kwa kuwa mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 Yeye aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami ndani yake.
57 Kama Baba mwenye uzima alivyonituma, na kama niishivyo kwa sababu ya Baba, na yeye pia ataishi kwa sababu yangu.
58 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, sio kama vile mababa walivyo kula wakafa. Yeye aulaye mkate huu ataishi milele.
59 Yesu aliyasema mambo haya ndani ya sinagogi alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu.
60 Ndipo wengi wa wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, “Hili nifundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?”
61 Yesu kwa sababu alijua ya kuwa wanafunzi wake walikuwa wakilinung'unikia jambo hili, akawambia je jambo hili linawakwaza?
62 Basi itakuaje mtakapomwona mwana wa Adamu akishuka kutoka alikokuwa kabla?
63 Ni Roho ndiye atoaye uzima. Mwili haufaidii kitu chochote. Maneno niliyoyasema kwenu ni roho na ni uzima.
64 Bado kuna watu kati yenu wasioamini.” kwa sababu Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti.
65 Akawambia, ni kwa sababu hii niliwambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba.”
66 Baada ya haya wanafunzi wake wengi walirudi nyuma na hawakuambatana naye tena.
67 Yesu akawambia wale kumi na wawili, “Je na ninyi mnataka kuondoka?”
68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele,
69 na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu.”
70 Yesu akawambia, “Je mimi sikuwachagua ninyi, na mmoja wenu ni ibilisi?
Yohana 6 in Biblia ya Kiswahili