Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 5:6-17 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 5:6-17 in Biblia Takatifu

6 Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo, akatambua kwamba alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, “Je, wataka kupona?”
7 Naye akajibu, “Mheshimiwa, mimi sina mtu wa kunipeleka majini wakati yanapotibuliwa. Kila nikijaribu kuingia, mtu mwingine hunitangulia.”
8 Yesu akamwambia, “Inuka, chukua mkeka wako utembee.”
9 Mara huyo mtu akapona, akachukua mkeka wake, akatembea. Jambo hili lilifanyika siku ya Sabato.
10 Kwa hiyo baadhi ya Wayahudi wakamwambia huyo mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali kubeba mkeka wako.”
11 Lakini yeye akawaambia, “Yule mtu aliyeniponya ndiye aliyeniambia: Chukua mkeka wako, tembea.”
12 Nao wakamwuliza, “Huyo mtu aliyekwambia: Chukua mkeka wako, tembea, ni nani?”
13 Lakini yeye hakumjua huyo mtu aliyemponya, maana Yesu alikuwa amekwisha ondoka mahali hapo, kwani palikuwa na umati mkubwa wa watu.
14 Basi, baadaye Yesu alimkuta huyo aliyeponywa Hekaluni, akamwambia, “Sasa umepona; usitende dhambi tena, usije ukapatwa na jambo baya zaidi.”
15 Huyo mtu akaenda, akawaambia viongozi wa Wayahudi kwamba Yesu ndiye aliyemponya.
16 Kwa vile Yesu alifanya jambo hilo siku ya Sabato, Wayahudi walianza kumdhulumu.
17 Basi, Yesu akawaambia, “Baba yangu anafanya kazi daima, nami pia nafanya kazi.”
Yohana 5 in Biblia Takatifu

Yohana 5:6-17 in Biblia ya Kiswahili

6 Yesu alipomwona amelala ndani ya matao na baada ya kutambua kuwa amelala pale kwa muda mrefu Yesu alimwambia, “Je unataka kuwa mzima?”
7 Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana sina mtu, wa kuniweka katika birika wakati maji yanapotibuliwa. Wakati ninapojaribu kuingia mtu mwingine hunitangulia.”
8 Yesu akamwambia, “Inuka na uchukue godoro lako na uende.”
9 Mara yule mtu akaponywa, akachukua kintanda chake na akaenda. Na siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.
10 Hivyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni siku ya Sabato, na hauruhusiwi kubeba godoro lako.”
11 Akajibu, yeye aliyeniponya ndiye aliyeniambia, “Chukua godoro lako na uende.”
12 Wakauliza, “Ni nani aliyekuambia 'Chukua godoro lako na uende?'''
13 Ingawa, yule aliyeponywa hakumjua, kwa sababu Yesu alikuwa ameondoka kwa siri. Kwa kuwa kulikuwa na watu wengi katika sehemu hiyo.
14 Baada ya hapo Yesu alimkuta yule mtu hekaluni na akamwambia, “Tazama, umepona! “Usitende dhambi tena usije ukapatwa na jambo baya zaidi.”
15 Yule mtu akaenda na kuwataarifu Wayahudi kuwa Yesu ndiye aliyemponya.
16 Hivyo, kwa sababu ya mambo hayo Wayahudi walimtesa Yesu, kwa sababu alifanya mambo haya siku ya Sabato.
17 Yesu akawambia, “Baba yangu anafanya kazi hata sasa nami nafanya kazi.”
Yohana 5 in Biblia ya Kiswahili