Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 5:28-45 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 5:28-45 in Biblia Takatifu

28 Msistaajabie jambo hili; maana wakati unakuja ambapo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake,
29 nao watafufuka: wale waliotenda mema watafufuka na kuishi, na wale waliotenda maovu watafufuka na kuhukumiwa.
30 “Mimi siwezi kufanya kitu kwa uwezo wangu mwenyewe. Mimi nina hukumu kama ninavyosikia kutoka kwa Baba, nayo hukumu yangu ni ya haki. Nia yangu si kufanya nipendavyo mwenyewe, bali apendavyo yule aliyenituma.
31 Nikijishuhudia mimi mwenyewe, ushahidi wangu hauwezi kukubaliwa kuwa wa kweli.
32 Lakini yuko mwingine ambaye hutoa ushahidi juu yangu, nami najua kwamba yote anayosema juu yangu ni ya kweli.
33 Ninyi mlituma ujumbe kwa Yohane naye aliushuhudia ukweli.
34 Si kwamba mimi nautegemea ushahidi wa wanadamu, lakini nasema mambo haya ili mpate kuokolewa.
35 Yohane alikuwa kama taa iliyokuwa ikiwaka na kuangaza, nanyi mlikuwa tayari kufurahia mwanga huo kwa kitambo.
36 Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.
37 Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake,
38 na ujumbe wake haukai ndani yenu maana hamkumwamini yule aliyemtuma.
39 Ninyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uzima wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia!
40 Hata hivyo, ninyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima.
41 “Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu.
42 Lakini nawajua ninyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.
43 Mimi nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu, lakini hamnipokei; bali mtu mwingine akija kwa mamlaka yake mwenyewe, mtampokea.
44 Mwawezaje kuamini, hali ninyi mnapenda kupokea sifa kutoka kwenu ninyi wenyewe, wala hamtafuti sifa kutoka kwake yeye aliye peke yake Mungu?
45 Msifikiri kwamba mimi nitawashtaki kwa Baba. Mose ambaye ninyi mmemtumainia ndiye atakayewashtaki.
Yohana 5 in Biblia Takatifu

Yohana 5:28-45 in Biblia ya Kiswahili

28 Msishangazwe na hili, kwa kuwa wakati unakuja ambao wafu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake
29 nao watatoka nje: kwa waliotenda mema kwa ufufuo wa uzima, na walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
30 Siwezi kufanya kitu chochote kutoka kwangu mwenyewe. Kama nisikiavyo, ndivyo ninavyo hukumu na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
31 Kama nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingelikuwa wa kweli.
32 Kuna mwingine anayeshuhudia kuhusu mimi na ninajua kwa hakika ushuhuda anaonishuhudia ni wa kweli.
33 Mmetuma kwa Yohana naye ameishuhudia kweli.
34 Hatahivyo, ushuhuda ninaoupokea hautoki kwa mwanadamu. Ninayasema haya ili kwamba mweze kuokolewa.
35 Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara, na mlikuwa tayari kuifurahia kwa muda kitambo nuru yake.
36 Ushuhuda nilionao ni mkuu kuliko ule wa Yohana, kwa kazi ambazo Baba amenipa kuzikamilisha, hizo kazi nizifanyazo zashuhudia kuwa Baba amenituma.
37 Baba aliyenituma yeye mwenyewe ameshuhudia kuhusu mimi. Hamjawahi kusikia sauti yake wala kuona umbo lake wakati wowote.
38 Hamna neno lake likikaa ndani yenu kwa kuwa hamumwamini yeye aliyetumwa.
39 Mnayachunguza maandiko mkidhani ndani yake mna uzima wa milele, na hayo maandiko yanashuhudia habari zangu na
40 hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima wa milele.
41 Sipokei sifa kutoka kwa watu,
42 lakini ninajua kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu ninyi wenyewe.
43 Nimekuja kwa jina la Baba yangu, hamukuweza kunipokea. Kama mwingine akija kwa jina lake mngempokea.
44 Je mnawezaje kuamini ninyi ambao mnapokea sifa kutoka kwa kila mmoja wenu lakini hamtafuti sifa itokayo kwa Mungu wa pekee?
45 Msidhani mimi nitawashitaki mbele za Baba. Anayewashitaki ninyi ni Musa, ambaye ninyi mmeweka matumaini yenu kwake.
Yohana 5 in Biblia ya Kiswahili