Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 2:6-12 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 2:6-12 in Biblia Takatifu

6 Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.
7 Yesu akawaambia, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza mpaka juu.
8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.”
9 Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi,
10 akamwambia, “Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!”
11 Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonyesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
12 Baada ya hayo, Yesu alishuka pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumu ambako walikaa kwa siku chache.
Yohana 2 in Biblia Takatifu

Yohana 2:6-12 in Biblia ya Kiswahili

6 Basi kulikuwa na mitungi sita ya mawe pale iliyowekwa kwa ajili ya kunawa katika sikukuu za Wayahudi, kila moja lilikuwa na ujazo wa nzio mbili tatu.
7 Yesu akawambia, “Ijazeni maji mitungi ya mawe.” Wakajaza hadi juu.
8 Kisha akawambia wale watumishi, “Chukueni kiasi sasa na mpeleke kwa muhudumu mkuu wa meza.” Wakafanya kama walivyoagizwa.
9 Mhudumu mkuu aliyaonja yale maji yaliyokuwa yamebadilika na kuwa divai, ila hakujua yalikotoka (lakini watumishi waliochota maji walijua yalikotoka). Kisha akamwita bwana harusi na
10 kumwambia, “Kila mmoja huanza kuwahudumia watu divai nzuri na wakiishalewa huwapa divai isiyo nzuri. Lakini wewe umeitunza divai nzuri hadi sasa”
11 Muujiza huu wa Kana ya Galilaya, ulikuwa ndio mwanzo wa ishara za miujiza aliyoifanya Yesu, akifunua utukufu wake, hivyo wanafunzi wake wakamwamini.
12 Baada ya hii, Yesu, mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake walienda katika mji wa Kapernaum na wakaa huko kwa siku chache.
Yohana 2 in Biblia ya Kiswahili