Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 21:20-24 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 21:20-24 in Biblia Takatifu

20 Hapo Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda, anafuata (Huyu mwanafunzi ndiye yule ambaye wakati wa chakula cha jioni, alikaa karibu sana na Yesu na kumwuliza: “Bwana ni nani atakayekusaliti?”)
21 Basi, Petro alipomwona huyo akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?”
22 Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini? Wewe nifuate mimi.”
23 Basi, habari hiyo ikaenea miongoni mwa wale ndugu kwamba mwanafunzi huyo hafi. Lakini Yesu hakumwambia kwamba mwanafunzi huyo hafi, ila, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini?”
24 Huyo ndiye yule aliyeshuhudia mambo haya na kuyaandika. Nasi twajua kwamba aliyoyasema ni kweli.
Yohana 21 in Biblia Takatifu

Yohana 21:20-24 in Biblia ya Kiswahili

20 Petro aligeuka na kumwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akawafuata- Huyu ndiye aliyekuwa amajiegemeza kwenye kifua cha Yesu wakati wa chakula cha jioni na kumwuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”
21 Petro alimwona na kisha akamwuliza Yesu, “Bwana, Huyu mtu atafanya nini?”
22 Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, hilo linakuhusu nini?” Nifuate.”
23 Kwa hiyo habari hii ikaenea miongoni mwa wale ndugu, kwamba mwanafunzi huyo hatakufa. Lakini Yesu hakumwambia Petro kuwa, mwanafunzi huyo hafi, “Kama nataka yeye abaki mpaka nitakapokuja yakuhusu nini?”
24 Huyu ndiye mwanafunzi atoaye ushuhuda wa mambo haya, na ndiye aliye andika mambo haya, na tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
Yohana 21 in Biblia ya Kiswahili