Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 21:15-21 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 21:15-21 in Biblia Takatifu

15 Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi zaidi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza wana kondoo wangu.”
16 Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”
17 Akamwuliza mara ya tatu, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Hapo Petro akahuzunika kwa sababu alimwuliza mara ya tatu: “Wanipenda?” akamwambia, “Bwana, wewe wajua yote; wewe wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu!
18 Kweli nakwambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda.”
19 (Kwa kusema hivyo, alionyesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu.) Kisha akamwambia, “Nifuate.”
20 Hapo Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda, anafuata (Huyu mwanafunzi ndiye yule ambaye wakati wa chakula cha jioni, alikaa karibu sana na Yesu na kumwuliza: “Bwana ni nani atakayekusaliti?”)
21 Basi, Petro alipomwona huyo akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?”
Yohana 21 in Biblia Takatifu

Yohana 21:15-21 in Biblia ya Kiswahili

15 Baada ya kuwa wamefungua kinywa, Yesu akamwambia Simon Petro, “Simon mwana wa Yohana je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana; “Wewe wajua kuwa mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wanakondoo wangu.”
16 Akamwambia mara ya pili, “Simon mwana wa Yona, je, wanipenda?” Petro akamwambia, “Ndiyo, Bwana; wewe wajua kuwa nakupenda. “Yesu akamwambia, “Chunga kondoo wangu.”
17 Akamwambia tena mara ya tatu, “Simon, mwana wa Yohana, Je wanipenda?” Naye Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, “Je Wewe wanipenda?” Naye akamwambia, “Bwana, unajua yote; unajua kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
18 Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda.”
19 Yesu alisema haya ili kuonesha ni aina gani ya kifo ambacho Petro angemtukuza Mungu. Baada ya kuwa amesema haya, akamwambia Petro, “Nifuate.”
20 Petro aligeuka na kumwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akawafuata- Huyu ndiye aliyekuwa amajiegemeza kwenye kifua cha Yesu wakati wa chakula cha jioni na kumwuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”
21 Petro alimwona na kisha akamwuliza Yesu, “Bwana, Huyu mtu atafanya nini?”
Yohana 21 in Biblia ya Kiswahili