Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 19:7-10 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 19:7-10 in Biblia Takatifu

7 Wayahudi wakamjibu, “Sisi tunayo Sheria, na kufuatana na Sheria hiyo, ni lazima afe, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.”
8 Pilato aliposikia maneno hayo akazidi kuogopa.
9 Basi, akaingia tena ndani ya ikulu, akamwuliza Yesu, “Umetoka wapi wewe?” Lakini Yesu hakumjibu neno.
10 Hivyo Pilato akamwambia, “Husemi nami? Je, hujui kwamba ninayo mamlaka ya kukufungua na mamlaka ya kukusulubisha?”
Yohana 19 in Biblia Takatifu

Yohana 19:7-10 in Biblia ya Kiswahili

7 Wayahudi wakamjibu Pilato, “Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu.”
8 Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa,
9 akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, “Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu.
10 Kisha Pilato akamwambia, “Je, wewe huongei na mimi? Je, wewe hujui kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua na mamlakaya kukusulubisha?”
Yohana 19 in Biblia ya Kiswahili