Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 19:4-9 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 19:4-9 in Biblia Takatifu

4 Pilato akatoka tena nje, akawaambia, “Tazameni, namleta nje kwenu, mpate kujua kwamba mimi sikuona hatia yoyote kwake.”
5 Basi, Yesu akatoka nje amevaa taji ya miiba na joho la rangi ya zambarau. Pilato akawaambia, “Tazameni! Mtu mwenyewe ni huyo.”
6 Makuhani wakuu na walinzi walipomwona wakapaaza sauti: “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni basi, ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa maana mimi sikuona hatia yoyote kwake.”
7 Wayahudi wakamjibu, “Sisi tunayo Sheria, na kufuatana na Sheria hiyo, ni lazima afe, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.”
8 Pilato aliposikia maneno hayo akazidi kuogopa.
9 Basi, akaingia tena ndani ya ikulu, akamwuliza Yesu, “Umetoka wapi wewe?” Lakini Yesu hakumjibu neno.
Yohana 19 in Biblia Takatifu

Yohana 19:4-9 in Biblia ya Kiswahili

4 Kisha Pilato alitoka nje na kuwaambia watu, “Tazama nawaleteeni huyu mtu kwenu ili mjue kwamba mimi sikuona hatia yoyote ndani yake.”
5 Kwa hiyo Yesu akatoka nje; alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau. Ndipo Pilato akawaambia, “Tazameni mtu huyu hapa!”
6 Kwa hiyo wakati kuhani mkuu na wakuu walipomwona Yesu, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe, msulubishe.” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa kuwa mimi sioni hatia ndani yake.”
7 Wayahudi wakamjibu Pilato, “Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu.”
8 Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa,
9 akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, “Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu.
Yohana 19 in Biblia ya Kiswahili