Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 19:29-38 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 19:29-38 in Biblia Takatifu

29 Hapo palikuwa na bakuli limejaa siki. Basi, wakachovya sifongo katika hiyo siki, wakaitia juu ya ufito wa husopo, wakamwekea mdomoni.
30 Yesu alipokwisha pokea hiyo siki, akasema, “Yametimia!” Kisha akainama kichwa, akatoa roho.
31 Ilikuwa Ijumaa, siku ya Maandalio. Kwa hiyo, kusudi miili isikae msalabani siku ya Sabato, maana siku hiyo ya Sabato ilikuwa siku kubwa, Wayahudi walimwomba Pilato miguu ya hao waliosulubiwa ivunjwe na miili yao iondolewe.
32 Basi, askari walikwenda, wakaivunja miguu ya yule mtu wa kwanza na yule wa pili ambao walikuwa wamesulubiwa pamoja na Yesu.
33 Lakini walipomfikia Yesu waliona kwamba alikwisha kufa, na hivyo hawakumvunja miguu.
34 Lakini askari mmoja alimtoboa ubavuni kwa mkuki, na mara ikatoka damu na maji.
35 (Naye aliyeona tukio hilo ametoa habari zake ili nanyi mpate kuamini. Na hayo aliyosema ni ukweli, tena yeye anajua kwamba anasema ukweli.)
36 Jambo hilo lilitendwa ili Maandiko Matakatifu yatimie: “Hapana hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.”
37 Tena Maandiko mengine yanasema: “Watamtazama yule waliyemtoboa.”
38 Baada ya hayo, Yosefu, mwenyeji wa Armathaya, alimwomba Pilato ruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. (Yosefu alikuwa mfuasi wa Yesu, lakini kwa siri, maana aliwaogopa viongozi wa Wayahudi). Basi, Pilato akamruhusu. Hivyo Yosefu alikwenda, akauondoa mwili wa Yesu.
Yohana 19 in Biblia Takatifu

Yohana 19:29-38 in Biblia ya Kiswahili

29 Chombo kilichokuwa kimejaa Siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake.
30 Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, “Imekwisha.” Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.
31 Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale wliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe.
32 Ndipo askari walipokuja na kuvunja miguu ya mtu wa kwanza na wa pili aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.
33 Walipomfikia Yesu, walimkuta tayari alikuwa amekwisha kufa, kwa hiyo hawakuvunja miguu yake.
34 Hata hivyo, mmoja wa askari alimchoma Yesu ubavuni kwa mkuki, na mara yakatoka maji na damu.
35 Naye aliyeona hili ametoa ushuhuda, na ushuhuda wake ni wa kweli. Yeye anajua kuwa alichokisema ni cha kweli ili nanyi pia muamini.
36 Mambo haya yalikuwa ili lile neno lililonenwa lipate kutimia, “Hakuna hata wake mmoja utakaovunjwa.”
37 Tena andiko lingine husema, “Watamtazama yeye waliyemchoma”
38 Baada ya mambo haya Yusufu wa Arimathaya, kwa vile alikuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri kwa kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato kwamba auchukue mwili wa Yesu. Naye Pilato akampa ruhusa. Kwa hiyo Yusufu akaja kuuondoa mwili wa Yesu.
Yohana 19 in Biblia ya Kiswahili