Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 19:13-30 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 19:13-30 in Biblia Takatifu

13 Basi, Pilato aliposikia maneno hayo akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo: “Sakafu ya Mawe” (kwa Kiebrania, Gabatha).
14 Ilikuwa yapata saa sita mchana, siku ya maandalio ya Pasaka. Pilato akawaambia Wayahudi, “Tazameni, Mfalme wenu!”
15 Wao wakapaaza sauti: “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!” Makuhani wakuu wakajibu, “Sisi hatuna Mfalme isipokuwa Kaisari!”
16 Basi, hapo Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulubiwe. Basi, wakamchukua Yesu.
17 Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa”, (kwa Kiebrania Golgotha).
18 Hapo ndipo walipomsulubisha, na pamoja naye waliwasulubisha watu wengine wawili; mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto, naye Yesu katikati.
19 Pilato aliandika ilani akaiweka juu ya msalaba. Nayo ilikuwa imeandikwa hivi: “Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi.”
20 Wayahudi wengi waliisoma ilani hiyo, maana mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji. Tena ilani hiyo ilikuwa imeandikwa kwa Kiebrania, Kilatini, na Kigiriki.
21 Basi, makuhani wakuu wakamwambia Pilato, “Usiandike: Mfalme wa Wayahudi, ila Yeye alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.”
22 Pilato akajibu, “Niliyoandika, nimeandika!”
23 Askari walipokwisha msulubisha Yesu, walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bila mshono.
24 Basi, hao askari wakashauriana: “Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani.” Jambo hilo lilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: “Waligawana mavazi yangu, na nguo yangu wakaipigia kura.” Basi, ndivyo walivyofanya hao askari.
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene.
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.”
27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
28 Yesu alijua kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.”
29 Hapo palikuwa na bakuli limejaa siki. Basi, wakachovya sifongo katika hiyo siki, wakaitia juu ya ufito wa husopo, wakamwekea mdomoni.
30 Yesu alipokwisha pokea hiyo siki, akasema, “Yametimia!” Kisha akainama kichwa, akatoa roho.
Yohana 19 in Biblia Takatifu

Yohana 19:13-30 in Biblia ya Kiswahili

13 Pilato alipoyasikia maneno haya, akamleta Yesu nje kisha akakaa kwenye kiti cha hukumu mahali pale panapojulikana kama sakafu, lakini kwa Kiebrania, Gabatha.
14 Siku ya maandalizi ya pasaka ilipofika, panapo muda wa saa ya sita. Pilato akawaambia Wayahudi, “Tazameni mfalme wenu huyu hapa!”
15 Wakapiga kelele, “Mwondoshe, mwondoshe, msulubishe!” Pilato akawaambia, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?” Naye Kuhani mkuu akajibu, “Sisi hatuna mfalme isipokuwa Kaisari.”
16 Ndipo Pilato alipomtoa Yesu kwao ili asulibiwe.
17 Nao wakamchukua Yesu, naye akatoka, hali ameubeba msalaba wake mwenyewe mpaka kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa, kwa Kihebrania huitwa Golgotha.
18 Ndipo walipomsulibisha Yesu, pamoja naye wanaume wawili, mmoja upende huu na mwingine upande huu, na Yesu katikati yao.
19 Kisha Pilato akaandika alama na kuiwekwa juu ya msalaba. Hapo paliandikwa: YESU MNAZARETH, MFALME WA WAYAHUDI.
20 Wengi wa Wayahudi waliisoma alama hiyo kwani mahali pale aliposulibishwa Yesu palikuwa karibu na mji. Alama hiyo iliadikwa kwa Kiebrania, kwa Kirumi na kwa Kiyunani.
21 Kisha wakuu wa makuhani wa Wayahudi wakamwambia Pilato, “Usiandike, 'Mfalme wa Wayahudi; bali yeye alisema mimi ni mfalme wa Wayahudi.”
22 Naye Pilato akawajibu, “Niliyoandika nimeandika.”
23 Baada ya askari kumsulibisha Yesu, walichukua mavazi yake na kuyagawa katika mafungu manne, kila askari fungu moja, vivyo hivyo na kanzo, Sasa ile kanzu haikuwa imeshonwa bali ilkuwa imefumwa yote tokea juu.
24 Kisha wakasemezana wao kwa wao, “Tusiipasue, bali tupigeni kura ili kuona itakuwa ya nani.” Hili lilitokea ili lile andiko litimizwe, lile lisemalo waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura.”
25 Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.
26 Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!”
27 Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.
28 Baada ya hilo, Hali Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, “Naona kiu.”
29 Chombo kilichokuwa kimejaa Siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake.
30 Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, “Imekwisha.” Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.
Yohana 19 in Biblia ya Kiswahili