Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 18:9-12 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 18:9-12 in Biblia Takatifu

9 (Alisema hayo ili yapate kutimia yale aliyosema: “Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja.”)
10 Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani Mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.
11 Basi, Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako alani. Je, nisinywe kikombe alichonipa Baba?”
12 Kile kikosi cha askari, mkuu wake na walinzi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga
Yohana 18 in Biblia Takatifu

Yohana 18:9-12 in Biblia ya Kiswahili

9 Haya yalikuwa hivyo ili lile neno litimilike; pale aliposema; “Katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja.”
10 Ndipo Simon Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani mkuu. Na jina lake mtumishi yule lilikuwa Malko.
11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?”
12 Basi lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi, walimkamata Yesu na kumfunga.
Yohana 18 in Biblia ya Kiswahili