Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 18:27-32 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 18:27-32 in Biblia Takatifu

27 Petro akakana tena; mara jogoo akawika.
28 Basi, walimchukua Yesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwa alfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwa najisi.
29 Kwa hiyo, Pilato aliwaendea nje, akasema, “Mna mashtaka gani juu ya mtu huyu?”
30 Wakamjibu, “Kama huyu hangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako.”
31 Pilato akawaambia, “Haya, mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kufuatana na Sheria yenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi hatuna mamlaka ya kumwua mtu yeyote.”
32 (Ilifanyika hivyo yapate kutimia maneno aliyosema Yesu kuonyesha atakufa kifo gani.)
Yohana 18 in Biblia Takatifu

Yohana 18:27-32 in Biblia ya Kiswahili

27 Petro akakana tena, na mara Jogoo akawika.
28 Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika na kuila pasaka.
29 Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. “Ni shitaka gani linalomhusu huyu mtu?”
30 Wakamjibu na kumwambia, “Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.”
31 Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria yenu.” Nao Wayahudi wakamwambia, “Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote.”
32 Walisema haya ili neno la Yesu litimilike, neno ambalo alikuwa amekwisha sema juu ya aina ya kifo chake.
Yohana 18 in Biblia ya Kiswahili