Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 11:12-31 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 11:12-31 in Biblia Takatifu

12 Wanafunzi wake wakamwambia, “Bwana, ikiwa amelala, basi atapona.”
13 Wao walidhani kwamba alikuwa amesema juu ya kulala usingizi, kumbe alikuwa amesema juu ya kifo cha Lazaro.
14 Basi, Yesu akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa;
15 Lakini nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini. Haya, twendeni kwake.”
16 Thoma (aitwaye Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, “Twendeni nasi tukafe pamoja naye!”
17 Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne.
18 Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu umbali upatao kilomita tatu.
19 Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao.
20 Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani.
21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!
22 Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”
23 Yesu akamwambia, “Kaka yako atafufuka.”
24 Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.”
25 Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uzima. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi:
26 na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?”
27 Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana! Naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.”
28 Baada ya kusema hayo, Martha alikwenda kumwita Maria, dada yake, akamwabia faraghani, “Mwalimu yuko hapa, anakuita.”
29 Naye aliposikia hivyo, akainuka mara, akamwendea Yesu.
30 Yesu alikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa bado mahali palepale Martha alipomlaki.
31 Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.
Yohana 11 in Biblia Takatifu

Yohana 11:12-31 in Biblia ya Kiswahili

12 Ndipo wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala, ataamka.
13 Wakati huu Yesu alikuwa akizungumza habari za kifo cha Lazaro, lakini wao walidhani anazungumza juu ya kulala usingizi.
14 Ndipo Yesu akazungumza nao wazi wazi, “Lazaro amekufa.
15 Nina furaha kwa ajili yenu, kwamba sikuwepo kule ili kwamba mpate kuamini. Twendeni kwake.”
16 Basi Tomaso, aliyeitwa Pacha, aliwaambia wanafunzi wenzake, “Nasi twendeni pia tukafe pamoja na Yesu.”
17 Wakati Yesu alipokuja, alikuta kwamba Lazaro tayari amekwishakuwa kaburini siku nne.
18 Nayo Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu kama kilomita arobaini na tano hivi.
19 Wengi kati ya Wayahudi wakaja kwa Martha na Mariamu kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.
20 Ndipo Martha aliposikia kuwa Yesu anakuja, alienda kukutana naye, lakini Mariamu aliendelea kukaa nyumbani.
21 Ndipo Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungelikuwa hapa, kaka yangu asingelikufa.
22 Hata sasa, najua ya kuwa lolote utakaloomba kutoka kwa Mungu, atakupatia.”
23 Yesu akamwambia, kaka yako atafufuka tena.”
24 Martha akamwambia, najua kwamba atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.”
25 Yesu akamwambia, “Mimi ni ufufuo na uzima; yeye aniaminiye, ingawa atakufa, hata hivyo atakuwa anaishi;
26 na yeye aishiye na kuniamini mimi hatakufa. Unaamini hili?”
27 Akamwambia, “Ndiyo, Bwana naamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, yeye ajaye katika ulimwengu.”
28 Alipokwisha kusema hili, alienda zake na kumwita dada yake Mariamu faraghani. Akasema, “Mwalimu yuko hapa na anakuita.”
29 Mariamu aliposikia haya, aliinuka kwa haraka na kwenda kwa Yesu.
30 Naye Yesu alikuwa hajaja bado ndani ya kijiji, bali alikuwa bado mahali alipokutana na Martha.
31 Ndipo Wayahudi waliokuwa na Mariamu katika nyumba na wale waliokuwa wakimfariji, walipomuona akiinuka haraka na kutoka nje, walimfuata; walidhani kuwa anaenda kaburini ili akalie huko.
Yohana 11 in Biblia ya Kiswahili