5 Mimi ni mweusi lakini mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, muzuri kama mapazia ya Sulemani.
6 Usinishangae kwasababu ni mweusi, kwasababu jua limeniunguza. Wana wa mama yangu walikuwa na hasira juu yangu; walinifanya mtunzi wa mashamba ya mizabibu, lakini mshamba langu la mizabibu sijatunza. Wanamke akizungumza na mpenzi wake.
7 Niambie, wewe ninaye kupenda, wapi unalisha mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye akangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu
8 Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji.
9 Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wakike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao.
10 Mashavu yako ni mazuri na mapambo, shingo yako na mikufu ya madini.
11 Nitakufanyia mapambo ya dhahabu yaliochanganywa na fedha. Mwanamke akiongea mwenyewe.
12 Wakati mfalme akiwa amelala kitandani mwake, marashi yangu yakasambaza arufu.
13 Mpenzi wangu ni kwangu kama mkebe wa marashi unao lala usiku katika ya maziwa yangu.
14 Mpenzi wangu ni kwangu kama kifurushi cha maua ya hena katika mashamba ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi wake anazungumza naye
15 Ona, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; ona, wewe ni mzuri; macho yako ni kama ya hua. Mwanamke anazungumza na mpenzi wake.
16 Ona, wewe ni mtanashati, mpenzi wangu, jinsi mtanashati.