Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waraka wa Yakobo

Waraka wa Yakobo 4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ugonvi na migogoro miongoni mwenu vyatoka wapi? Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu?
2Mnatamani kile msichokuwa nacho. Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho. Mnapigana na kugombana, na bado hampati kwa sababu hamumwombi Mungu.
3Mnaomba na hampokei kwa sababu mnaomba kwa ajili ya mambo mabaya, ili kwamba muweze kuvitumia kwa tamaa zenu mbaya.
4Enyi wazinzi! Hamjui kwamba urafiki na ulimwengu ni uadui dhidi ya Mungu? Kwa hiyo, yeyote aamuaye kuwa rafiki wa ulimwengu hujifanya mwenyewe adui wa Mungu.
5Au mnadhani maandiko hayana maana yasemapo kwamba Roho aliyoweka ndani yetu ana wivu sana kwa ajili yetu?
6Lakini Mungu hutoa neema zaidi, ndiyo maana maandiko husema, “Mungu humpinga mwenye kiburi, lakini humpa neema mnyenyekevu.”
7Hivyo, jitoeni kwa Mungu. Mpingeni ibilisi na yeye atakimbia kutoka kwenu.
8Sogeeni karibu na Mungu, na yeye atakaribia karibu nanyi. Safisheni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na takaseni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
9Huzunikeni, ombolezeni, na kuria! Geuzeni kicheko chenu kuwa huzuni na furaha yenu kuwa maombolezo.
10Jinyenyekezeni wenyewe mbele za Bwana, na atawainua juu.
11Msineneane kinyume ninyi kwa ninyi, ndugu. Mtu anenaye kinyume na ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, hunena kinyume na sheria na huihukumu sheria ya Mungu. Mkiihukumu sheria, hamuitii sheria, bali mnaihukumu.
12Ni mmoja tu ambaye ni mtoa sheria na hakimu, Mungu, yeye ambaye ana uwezo wa kuokoa na kuangamiza. Wewe ni nani ambaye unamhukumu jirani yako?
13Sikilizeni, ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu, na kukaa mwaka huko, na kufanya biashara, na kutengeneza faida.”
14Ni nani ajuaye nini kitatokea kesho, na maisha yenu ni nini hasa? Kwa kuwa mnafanana kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi na kisha hupotea.
15Badala yake mngesema, “kama ni mapenzi ya Bwana, tutaishi na tutafanya hiki au kile.”
16Lakini sasa mnajivuna juu ya mipango yenu. Majivuno yote hayo ni uovu.
17Kwahiyo, kwake yeye ajuaye kutenda mema lakini hayatendi, kwake huyo ni dhambi.