28 Je mtu anaweza kutembea juu ya makaa bila kuchomwa miguu yake?
29 Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa jirani yake; yule alalaye na huyo mke hatakosa adhabu.
30 Watu hawawezi kumdharau mwizi kama anaiba ili kukidhi hitaji lake la njaa.
31 Walakini akimatwa, atalipa mara saba ya kile alichoiba; lazima atoe kila kitu cha thamani katika nyumba yake.
32 Mtu anayefanya uzinzi hana akili; hufanya hiyo kwa uharibifu wake mwenyewe.
33 Anasitahili aibu na majeraha na fedheha yake haiwezi kuondolewa.
34 Maana vivu humghadhibisha mtu; hatakuwa na huruma wakati wa kulipa kisasi chake.