Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 6:11-29 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 6:11-29 in Biblia ya Kiswahili

11 ndipo umasikini wako utakapokujia kama mporaji na uhitaji wako kama askari wa vita.
12 Mtu asiyefaa-mtu mwovu- huishi kwa kauli za udanganyifu wake,
13 akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake.
14 Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka.
15 Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona.
16 Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.
17 Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu,
18 moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi,
19 shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu.
20 Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21 Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako.
22 utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha.
23 Maana amri ni taa, na mafundisho ni nuru; kinga za kuadilisha za njia ya uzima.
24 Yanakulinda dhidi ya mwanamke malaya, dhidi ya maneno laini ya uzinzi.
25 Moyoni mwako usiutamani uzuri wake wala usitekwe katika kope zake.
26 Kulala na malaya inaweza kugharimu bei ya kipande cha mkate, lakini mke wa mtu mwingine inagharimu uzima wako wote.
27 Je mtu anaweza kubeba moto katika kifua chake bila kuuguza mavazi yake?
28 Je mtu anaweza kutembea juu ya makaa bila kuchomwa miguu yake?
29 Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa jirani yake; yule alalaye na huyo mke hatakosa adhabu.
Mithali 6 in Biblia ya Kiswahili