Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 4:10-17 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 4:10-17 in Biblia ya Kiswahili

10 Mwanangu, sikiliza, na kuzingatia maneno yangu, nawe utapata miaka mingi ya maisha yako.
11 Ninakuelekeza katika njia ya hekima, nimekuongoza katika mapito yaliyonyooka.
12 Unapotembea, hakuna atakayesimama katika njia yako na kama ukikimbia hutajikwaa.
13 Shika mwongozo wala usiuache, utakuongoza, maana ni uzima wako.
14 Usifuate njia ya waovu wala usiende katika njia ya watendao uovu.
15 Jiepushe nayo, usipite katika njia hiyo; geuka na upite njia nyingine.
16 Maana hawawezi kulala mpaka wafanye ubaya na hupotewa na usingizi hadi wasababishe mtu kujikwaa.
17 Maana wao hula mkate wa uovu na hunywa divai ya vurugu.
Mithali 4 in Biblia ya Kiswahili