Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 2:9-19 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 2:9-19 in Biblia ya Kiswahili

9 Ndipo utakapoelewa wema, haki, usawa na kila njia njema.
10 Maana hekima itaingia moyoni mwako na maarifa yataipendeza nafsi yako.
11 Busara itakulinda, ufahamu utakuongoza.
12 Vitakuokoa kutoka katika njia ya uovu, kutoka kwa wale waongeao mambo potovu.
13 Ambao huziacha njia za wema na kutembea katika njia za giza.
14 Hufurahia wanapotenda maovu na hupendezwa katika upotovu.
15 Hufuata njia za udanganyifu na kwa kutumia ghilba huficha mapito yao.
16 Busara na hekima zitakuokoa kutoka kwa mwanamke malaya, kutoka kwa mwanamke anayetafuta visa na mwenye maneno ya kubembeleza.
17 Yeye humwacha mwenzi wa ujana wake na kusahau agano la Mungu wake.
18 Maana nyumba yake huinama na kufa na mapito yake yatakupeleka kwa wale walioko kaburini.
19 Wote waiendeao njia yake hawatarudi tena na wala hawataziona njia za uzima.
Mithali 2 in Biblia ya Kiswahili