Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 23:13-25 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 23:13-25 in Biblia ya Kiswahili

13 Usizuie kuadilisha mtoto, maana ukimchapa kwa fimbo, hatakufa.
14 Ni wewe unayepaswa kumchapa kwa fimbo na kuikoa nafsi yake kuzimu.
15 Mwanangu, kama moyo wako una busara, basi moyo wangu utafurahi pia;
16 sehemu zangu ndani kabisa zitafurahi sana midomo yako inaponena haki.
17 Usiruhusu moyo wako kuwahusudu wenye dhambi, lakini endelea kumcha Yehova siku zote.
18 Hakika tumaini lako halitaondolewa na siku zako za hapo baadaye.
19 Sikia- wewe! - mwanangu, na uwe mwenye busara na uelekeze moyo wako katika njia.
20 Usishirikiane pamoja na walevi, au pamoja na walaji wa nyama walafi,
21 maana mlevi na mlafi wanakuwa masikini na usingizi utawavika kwa matambara.
22 Msikilize baba yako ambaye alikuzaa na usimdharau mama yako wakati akiwa mzee.
23 Inunue kweli, lakini usiiuze; nunua hekima, nidhamu, na ufahamu.
24 Baba yake mwenye haki atafurahia sana, na yule amzaaye mtoto mwenye busara atamfurahia.
25 Mfurahishe baba yako na mama yako na yule aliyekuzaa afurahie.
Mithali 23 in Biblia ya Kiswahili