Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 18:4-11 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 18:4-11 in Biblia ya Kiswahili

4 Maneno ya kinywa cha mtu ni maji yenye kina kirefu; chemchemi ya hekima ni mkondo unaotiririka.
5 Si vema kuwa na upendeleo kwa mwovu, wala haifai kukana haki kwa wale watendao mema.
6 Midomo ya mpumbavu huletea mafarakano na kinywa chake hukaribisha mapigo.
7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na hujinasa mwenye kwa midomo yake.
8 Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu na hushuka katika sehema za ndani sana kwenye mwili.
9 Basi, ambaye ni mzembe katika kazi yake ni ndugu yake anayeharibu wengi.
10 Jina la Yehova ni mnara imara; atendaye haki hukimbilia na kuwa salama.
11 Mali ya tajiri ni mji wake imara na katika fikira zake ni kama ukuta mrefu.
Mithali 18 in Biblia ya Kiswahili