Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 15:1-31 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 15:1-31 in Biblia ya Kiswahili

1 Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira.
2 Ulimi wa watu mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha wapumbavu humwaga upuuzi.
3 Macho ya Yehova yapo kila mahali, yakiwatazama juu ya waovu na wema.
4 Ulimi unaoponya ni mti wa uzima, bali ulimi wa udanganyifu huvunja moyo.
5 Mpumbavu hudharau marudi ya baba yake, bali yeye anayejifunza kutokana na masahihisho ni mwenye hekima.
6 Katika nyumba ya wale watendao haki kuna hazina kubwa, bali mapato ya watu waovu huwapa taabu.
7 Midomo ya wenye hekima husambaza maarifa, bali mioyo ya wapumbavu haifanyi hivyo.
8 Yehova anachukia sadaka za watu waovu, bali maombi ya watu waadilifu ndiyo furaha yake.
9 Yehova anachukia njia ya watu waovu, bali anampenda yule ambaye huandama haki.
10 Marudi ya ukatili hungojea kwa yeyote ambaye huiacha njia na yule ambaye huchukia masahihisho atakufa.
11 Kuzimu na uharibifu vipo wazi mbele za Yehova; je si zaidi sana mioyo ya wana wa wanadamu?
12 Mwenye mzaha huchukia masahihisho; hatakwenda kwa wenye hekima.
13 Moyo wenye furaha husababisha uchangamfu wa uso, bali huzuni huvunja moyo.
14 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha wapumbavu hujilisha kwenye upuuzi.
15 Siku zote za watu waliokandamizwa ni taabu, bali moyo wenye furaha unakaramu daima.
16 Bora kitu kidogo pamoja na kumcha Mungu kuliko hazina kubwa pamoja na ghasia.
17 Bora mlo wenye mboga kukiwa na upendo kuliko kuandaliwa ndama aliyenona kwa chuki.
18 Mtu mwenye hasira huchochea mabishano, bali mtu ambaye hukawia kukasirika hutuliza ugomvi.
19 Mapito ya mtu goigoi ni kama sehemu yenye uwa wa miiba, bali mapito ya mtu mwadilifu ni njia kuu iliyojengwa imara.
20 Mwana mwenye busara huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.
21 Upuuzi humfurahia mtu ambaye amepungukiwa akili, bali mwenye ufahamu hutembea katika njia nyofu.
22 Mipango huharibika ambapo hakuna ushauri, bali washauri wengi wanafanikiwa.
23 Mtu anapata furaha wakati anapotoa jibu la kufaa; je ni zuri kiasi gani neno kwa wakati muafaka!
24 Njia ya uzima huwapeleka juu watu wenye hekima, ili waondoke kutoka chini kuzimu.
25 Yehova hurarua urithi wa mwenye kiburi, bali huzilinda mali za mjane.
26 Yehova huyachukia mawazo ya watu waovu, bali maneno ya upole ni safi.
27 Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.
28 Moyo wa yule atendaye haki hutafakari kabla ya kujibu, bali kinywa cha watu waovu humwanga ubaya wake wote.
29 Yehova yupo mbali na watu waovu, bali husikia maombi ya wale watendao haki.
30 Nuru ya macho huleta furaha moyoni na habari njema ni afya kwenye mwili.
31 Kama utazingatia wakati mtu anapokurekebisha jinsi ya kuishi, utabaki miongoni mwa watu wenye busara.
Mithali 15 in Biblia ya Kiswahili