Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 27:9-19 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 27:9-19 in Biblia Takatifu

9 Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapa onyo:
10 “Waheshimiwa, nahisi kwamba safari hii itakuwa ya shida na hasara nyingi si kwa shehena na meli tu, bali pia kwa maisha yetu.”
11 Lakini yule ofisa alivutiwa zaidi na maoni ya nahodha na ya mwenye meli kuliko yale aliyosema Paulo.
12 Kwa kuwa bandari hiyo haikuwa mahali pazuri pa kukaa wakati wa baridi, wengi walipendelea kuendelea na safari, ikiwezekana mpaka Foinike. Foinike ni bandari ya Krete inayoelekea kusini-magharibi na kaskazini-magharibi; na huko wangeweza kukaa wakati wa baridi.
13 Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakang'oa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.
14 Lakini haukupita muda, upepo mkali uitwao “Upepo wa Kaskazi” ulianza kuvuma kutoka kisiwani.
15 Upepo uliipiga ile meli, na kwa kuwa hatukuweza kuukabili, tukaiacha ikokotwe na huo upepo.
16 Kisiwa kimoja kiitwacho Kanda kilitukinga kidogo na ule upepo; na tulipopita kusini mwake tulifaulu, ingawa kwa shida, kuusalimisha ule mtumbwi wa meli.
17 Wale wanamaji waliuvuta mtumbwi ndani, kisha wakaizungushia meli kamba na kuifunga kwa nguvu. Waliogopa kwamba wangeweza kukwama kwenye ufuko wa bahari, pwani ya Libya. Kwa hiyo walishusha matanga na kuiacha meli ikokotwe na upepo.
18 Dhoruba iliendelea kuvuma na kesho yake wakaanza kutupa nje shehena ya meli.
19 Siku ya tatu, wakaanza pia kutupa majini vifaa vya meli kwa mikono yao wenyewe.
Matendo 27 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 27:9-19 in Biblia ya Kiswahili

9 Tulikuwa tumechukua muda mwingi sana, na muda wa mfungo wa Kiyahudi ulikuwa umepita pia, na sasa ilikuwa ni hatari kuendelea kusafiri. Hivyo Paulo akatuonya,
10 na kusema, “Wanaume, naona safari ambayo tunataka tuichukue itakuwa na madhara na hasara nyingi, siyo tu ya mizigo na meli, lakini pia ya maisha yetu.”
11 Lakini afisa wa jeshi la Kiroma akamsikiliza zaidi bwana wake na mmiliki wa meli, kuliko mambo yale ambayo yalizungumzwa na Paulo.
12 Kwa sababu bandari haikuwa sehemu rahisi kukaa wakati wa baridi, mabaharia wengi wakashauri tusafiri kutoka pale, ili kwa namna yoyote tukiweza kuufikia mji wa Foinike, tukae pale wakati wa baridi. Foinike ni bandari huko Krete, na inatazama kaskazini mashariki na kusini mashariki.
13 Upepo wa kusini ulipoanza kuvuma polepole, mabaharia wakafikiri wamepata kile ambacho walikuwa wanakihitaji. Wakang'oa nanga na kusafiri kandokando ya Krete karibu na pwani.
14 Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali, ulioitwa Wa kaskazini mashariki, ukaanza kutupiga kutoka ng'ambo ya kisiwa.
15 Wakati meli ilipolemewa na kushindwa kuukabili upepo, tukakubaliana na hali hiyo, tukasafirishwa nao.
16 Tukakimbia kupitia ule upande uliokuwa unaukinga upepo wa kisiwa kiitwacho Kauda; na kwa taabu sana tulifanikiwa kuuokoa mtumbwi.
17 Baada ya kuwa wameivuta, walitumia kamba kuifunga meli. Waliogopa kwamba tungeweza kwenda kwenye eneo la mchanga mwingi la Syiti, hivyo wakashusha nanga na waliendeshwa kandokando.
18 Tulipigwa kwa nguvu sana na dhoruba, hivyo siku iliyofuata mabaharia wakaanza kutupa mizigo kutoka melini.
19 Siku ya tatu, mabaharia wakaanza kuyatoa maji kwa mikono yao wenyewe.
Matendo ya Mitume 27 in Biblia ya Kiswahili