1 Watu fulani walishuka kutoka Uyahudi na kuwafundisha ndugu, wakisema, “msipotahiriwa kama desturi ya Musa, hamwezi kuokolewa.”
2 Wakati Paulo na Barnaba walipokuwa na mapambano na mjadala pamoja nao, ndugu waliamua kwamba Paulo, Barnaba, na wengine kadhaa waende Yerusalem kwa mitume na wazee kwa ajili ya swali hili.
3 Kwa hiyo, kwa kutumwa kwao na kanisa, walipitia Foinike na Samaria wakitangaza kugeuzwa nia kwa wamataifa. Walileta furaha kuu kwa ndugu wote,
4 Walipokuja Yerusalem, walikaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, na waliwasilisha taarifa ya mambo yote ambayo Mungu amefanya pamoja nao.
5 Lakini watu fulani walioamini, waliokuwa katika kundi la Mafarisayo, walisimama nakusema, “ni muhimu kuwatahiri na kuwaamuru waishike sheria ya Musa.”
6 Hivyo mitume na wazee walisimama pamoja kulifikiria hili swala.