Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 10:8-21 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 10:8-21 in Biblia Takatifu

8 akawaeleza yote yaliyotukia, akawatuma Yopa.
9 Kesho yake, hao watu watatu wakiwa bado safarini, lakini karibu kufika Yopa, Petro alipanda juu ya paa la nyumba yapata saa sita mchana ili kusali.
10 Aliona njaa, akatamani kupata chakula. Chakula kilipokuwa kinatayarishwa, alipatwa na usingizi mzito akaona maono.
11 Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne.
12 Ndani ya shuka hiyo kulikuwa na kila aina ya wanyama: wanyama wenye miguu minne, wanyama watambaao na ndege wa angani.
13 Akasikia sauti ikimwambia: “Petro, amka uchinje, ule!”
14 Petro akajibu, “La, Bwana; mimi sijaonja kamwe chochote ambacho ni najisi au kichafu.”
15 Ile sauti ikasikika tena ikimwambia: “Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa!”
16 Jambo hili lilifanyika mara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juu mbinguni.
17 Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hilo maono alilokuwa ameliona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua nyumba ya Simoni, walifika mlangoni,
18 Wakaita kwa sauti: “Je, kuna mgeni humu aitwaye Simoni Petro?”
19 Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa lile maono, na hapo Roho akamwambia, “Sikiliza! kuna watu watatu hapa, wanakutafuta.
20 Shuka upesi na wala usisite kwenda pamoja nao kwa maana ni mimi niliyewatuma.”
21 Basi, Petro akateremka chini, akawaambia hao watu, “Mimi ndiye mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?”
Matendo 10 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 10:8-21 in Biblia ya Kiswahili

8 Kornelio aliwaambia yote yaliyotokea na akawatuma Yafa.
9 Siku iliyofuata muda wa saa sita wakiwa njiani na wamekaribia mjini, Petro akapanda juu darini kuomba.
10 Na pia akawa na njaa na alihitaji kitu cha kula, lakini wakati watu wanapika chakula, akaonyeshwa maono,
11 akaona anga limefuguka na chombo kinashuka na kitu fulani kama nguo kubwa ikishuka chini kwenye ardhi katika kona zake zote nne.
12 Ndani yake kulikuwa na aina zote za wanyama wenye miguu minne na watambaao juu ya ardhi, na ndege wa angani.
13 Tena sauti ikasema kwake “Amka, Petro chinja na ule”.
14 Lakini Petro akasema “Siyo hivyo, Bwana kwa sababu sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu.
15 Lakini sauti ikaja kwake tena kwa mara ya pili “Alichokitakasa Mungu usikiite najisi wala kichafu”.
16 Hii ilitokea mara tatu, na kile chombo kikawa kimechukuliwa tena angani.
17 Na wakati Petro akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa juu ya hayo maono yanamaanisha nini, Tazama, watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakasimama mbele ya lango, wakiuliza njia ya kwenda kwenye nyumba.
18 Na wakaita na kuuliza kama Simoni ambaye pia aliitwa Petro kama alikuwa anakaa pale.
19 Wakati huo Petro alipokuwa akiwaza juu ya hayo maono, Roho akasema naye, “Tazama watu watatu wanakutafuta.
20 Amka na ushuke chini na uende nao. Usiogope kwenda nao, kwa sababu nimewatuma.”
21 Petro akashuka chini kwao na kusema “Mimi ni yule mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?”
Matendo ya Mitume 10 in Biblia ya Kiswahili