Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 10:1-13 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 10:1-13 in Biblia Takatifu

1 Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, Jemadari wa kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha Italia.”
2 Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.
3 Yapata saa tisa mchana, aliona dhahiri katika maono malaika wa Mungu akiingia ndani na kumwambia, “Kornelio!”
4 Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia, “Kuna nini Mheshimiwa?” Huyo malaika akamwambia, “Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini.
5 Sasa, watume watu Yopa wakamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro.
6 Yeye yumo nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi ambaye nyumba yake iko karibu na bahari.”
7 Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye alikuwa mcha Mungu,
8 akawaeleza yote yaliyotukia, akawatuma Yopa.
9 Kesho yake, hao watu watatu wakiwa bado safarini, lakini karibu kufika Yopa, Petro alipanda juu ya paa la nyumba yapata saa sita mchana ili kusali.
10 Aliona njaa, akatamani kupata chakula. Chakula kilipokuwa kinatayarishwa, alipatwa na usingizi mzito akaona maono.
11 Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne.
12 Ndani ya shuka hiyo kulikuwa na kila aina ya wanyama: wanyama wenye miguu minne, wanyama watambaao na ndege wa angani.
13 Akasikia sauti ikimwambia: “Petro, amka uchinje, ule!”
Matendo 10 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 10:1-13 in Biblia ya Kiswahili

1 Kulikuwa na mtu fulani katika mji wa kaisaria, jina lake aliitwa Kornelio, alikuwa mkuu wa kikosi cha Kiitalia.
2 Alikuwa mchamungu na alimwabudu Mungu na nyumba yake yote; alitoa pesa nyingi kwa wayahudi na aliomba kwa Mungu siku zote.
3 Muda wa saa tisa za mchana, akaona maono Malaika wa Mungu anakuja kwake. Malaika akamwambia “Kornelio!
4 Kornelio akamwangalia malaika na alikuwa na hofu kubwa sana akasema “Hii ni nini mkuu?” Malaika akamwambia “Maombi yako na zawadi zako kwa masikini zimepanda juu kama kumbukumbu kwenye uwepo wa Mungu”.
5 Sasa tuma watu kwenda mji wa Yafa kumleta mtu mmoja anayeitwa Simoni ambaye pia huitwa Petro.
6 Anakaa na mtengenezaji wa Ngozi aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.”
7 Baada ya Malaika aliyekuwa akisema naye kuondoka, Kornelio akawaita watumishi wa nyumbani kwake wawili, na askari aliyekuwa akimwabudu Mungu kati ya maaskari waliokuwa wanamtumikia.
8 Kornelio aliwaambia yote yaliyotokea na akawatuma Yafa.
9 Siku iliyofuata muda wa saa sita wakiwa njiani na wamekaribia mjini, Petro akapanda juu darini kuomba.
10 Na pia akawa na njaa na alihitaji kitu cha kula, lakini wakati watu wanapika chakula, akaonyeshwa maono,
11 akaona anga limefuguka na chombo kinashuka na kitu fulani kama nguo kubwa ikishuka chini kwenye ardhi katika kona zake zote nne.
12 Ndani yake kulikuwa na aina zote za wanyama wenye miguu minne na watambaao juu ya ardhi, na ndege wa angani.
13 Tena sauti ikasema kwake “Amka, Petro chinja na ule”.
Matendo ya Mitume 10 in Biblia ya Kiswahili