Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 8:18-27 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 8:18-27 in Biblia Takatifu

18 Hapo Simoni aling'amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
19 “Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyote nitakayemwekea mikono, apokee Roho Mtakatifu.”
20 Lakini Petro akamjibu, “Potelea mbali na fedha zako kwa vile unafikiri kwamba unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!
21 Huna sehemu yoyote wala haki katika kazi hiyo kwa maana moyo wako hauko sawa mbele ya macho ya Mungu.
22 Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
23 Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na mfungwa wa dhambi!”
24 Simoni akajibu, “Tafadhali, niombeeni kwa Bwana lisije likanipata lolote kati ya hayo mliyosema.”
25 Baada ya Petro na Yohane kutoa ushuhuda wao na kuutangaza ujumbe wa Bwana, walirudi Yerusalemu. Walipokuwa wanarudi walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.
26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita jangwani.)
27 Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati huohuo kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea nyumbani. Huyo mtu alikuwa ofisa maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo alikuwa anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa.
Matendo 8 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 8:18-27 in Biblia ya Kiswahili

18 Wakati Simoni alipoona kwamba Roho Mtakatifu ametolewa kupitia kuwekewa mikono na mitume; akataka kuwapa pesa,
19 Akasema, “Nipeni hii nguvu, ili kila nitakayemwekea mikono apokee Roho Mtakatifu.”
20 Lakini Petro akamwambia; pesa yako pamoja na wewe ipotelee mbali, kwa sababu umedhani kuwa karama ya Mungu inapatikana kwa pesa.
21 Hauna sehemu katika jambo hili, kwa sababu moyo wako si mnyoofu mbele za Mungu.
22 Hivyo basi tubu maovu yako na kumwomba Mungu labda utasamehewe fikra za moyo wako.
23 Kwa maana naona uko katika sumu ya uchungu na kifungo cha dhambi.”
24 Simoni akajibu na kusema, “Mwombeni Bwana kwa ajili yangu, kwa kuwa mambo yote mliyozungumza yaweza kunitokea.
25 Wakati Petro na Yohana walipokuwa wameshuhudia na kuhubiri neno la Bwana, walirudi Yerusalemu kwa njia hiyo; walihubiri injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.
26 Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, “Angaza na uende kusini katika njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza.” (Njia hii iko katika jangwa).
27 Akaangaza na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya kandase; malkia wa Ethiopia. Aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu.
Matendo ya Mitume 8 in Biblia ya Kiswahili