Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 28:6-19 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 28:6-19 in Biblia Takatifu

6 Wale watu walikuwa wakitazamia kwamba angevimba au hapohapo angeanguka chini na kufa. Baada ya kungojea kwa muda mrefu bila kuona kwamba Paulo amepatwa na jambo lolote lisilo la kawaida, walibadilisha fikira zao juu yake, wakasema kuwa ni mungu.
7 Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya Publio, mkuu wa kile kisiwa. Publio alitukaribisha kirafiki, tukawa wageni wake kwa siku tatu.
8 Basi, ikawa kwamba baba yake Publio alikuwa amelala kitandani, mgonjwa, ana homa na kuhara. Paulo alikwenda kumwona na baada ya kusali, akaweka mikono yake juu ya mgonjwa, akamponya.
9 Kutokana na tukio hilo, wagonjwa wote katika kile kisiwa walikuja wakaponywa.
10 Watu walitupatia zawadi mbalimbali na wakati tulipoanza tena safari, walitia ndani ya meli masurufu tuliyohitaji.
11 Baada ya miezi mitatu tulianza tena safari yetu kwa meli moja ya Aleksandria iitwayo “Miungu Pacha”. Meli hiyo ilikuwa imetia nanga kisiwani wakati wote wa baridi.
12 Tulifika katika mji wa Sirakusa, tukakaa hapo kwa siku tatu.
13 Toka huko tuling'oa nanga, tukazunguka na kufika Regio. Baada ya siku moja, upepo ulianza kuvuma kutoka kusini, na baada ya siku mbili tulifika bandari ya Potioli.
14 Huko tuliwakuta ndugu kadhaa ambao walituomba tukae nao kwa juma moja. Hivi ndivyo tulivyopata kufika Roma.
15 Ndugu wa kule Roma walipopata habari zetu, wakaja kutulaki kwenye soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akapata moyo.
16 Tulipofika Roma, Paulo aliruhusiwa kukaa peke yake pamoja na askari mmoja wa kumlinda.
17 Baada ya siku tatu, Paulo aliwaita pamoja viongozi wa Kiyahudi wa mahali hapo. Walipokusanyika, Paulo aliwaambia, “Wananchi wenzangu, mimi, ingawa sikufanya chochote kibaya wala kupinga desturi za wazee wetu, nilitiwa nguvuni kule Yerusalemu na kutiwa mikononi mwa Waroma.
18 Waliponihoji na kuona kwamba sikuwa na hatia yeyote, walitaka kuniacha.
19 Lakini Wayahudi wengine walipinga jambo hilo, nami nikalazimika kukata rufani kwa Kaisari, ingawa sikuwa na chochote cha kuwashtaki wananchi wenzangu.
Matendo 28 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 28:6-19 in Biblia ya Kiswahili

6 Wao walimngojea avimbe kwa homa au aanguke ghafla na kufa. Lakini baada ya kumwangalia kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna jambo ambalo si la kawaida kwake, walibadilisha mawazo yao na kusema alikuwa mungu.
7 Basi mahali pale karibu palikuwa na ardhi ambayo ilikuwa mali ya mkuu wa kisiwa, mtu aliyeitwa Pablio. Alitukaribisha na kutukarimu kwa siku tatu.
8 Ilitokea kwamba baba wa Pablio alishikwa na homa na ugonjwa wa kuhara. Na Paulo alipomwendea, aliomba, akaweka mikono juu yake, na kumponya.
9 Baada ya hili kutokea, watu wengine pale kisiwani waliokuwa wanaumwa pia walikwenda na waliponywa.
10 Watu wakatuheshimu kwa heshima nyingi. Tulipokuwa tunajiandaa kusafiri, walitupa vile tulivyovihitaji.
11 Baada ya miezi mitatu, tulisafiri ndani ya meli ya Iskanda ambayo ilikuwa imepigwa baridi hapo kisiwani, ambayo viongozi wake walikuwa ndugu wawili mapacha.
12 Baada ya kuwa tumetua katika mji wa Sirakusa, tulikaa pale siku tatu.
13 Kutokea pale tulisafiri tukafika katika mji wa Regio. Baada ya siku moja upepo wa kusini ulitokea ghafla, na baada ya siku mbili tukafika katika mji wa Putoli.
14 Huko tuliwakuta baadhi ya ndugu na tulikaribishwa kukaa nao kwa siku saba. Kwa njia hii tukaja Rumi.
15 Kutoka huko wale ndugu, baada ya kuwa wamesikia habari zetu, walikuja kutupokea huko soko la Apias na Hotel tatu. Paulo alipowaona wale ndugu alimshukuru Mungu akajitia ujasiri.
16 Tulipoingia Roma, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake pamoja na yule askari aliyekuwa akimlinda.
17 Basi ilikuwa baada ya siku tatu Paulo aliwaita pamoja wale wanume waliokuwa viongozi kati ya Wayahudi. Walipokuja pamoja, alisema kwao, “Ndugu, pamoja na kwamba sijafanya kosa lolote kwa watu hawa au kufanya kinyume na taratibu za mababa zetu waliotutangulia, nilitolewa kama mfungwa kutoka Yerusalemu hadi kwenye mikono ya Warumi.
18 Baada ya kunihoji, walitamani kuniacha huru, kwa sababu kulikuwa hakuna sababu kwangu mimi ya kustahili adhabu ya kifo.
19 Lakini wale Wayahudi walipoongea kinyume cha shauku yao, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisaria, japokuwa haikuwa kana kwamba naleta mashtaka juu ya taifa langu.
Matendo ya Mitume 28 in Biblia ya Kiswahili