Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 24:8-12 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 24:8-12 in Biblia Takatifu

8 Kisha akaamuru washtaki wake waje mbele yako.
9 Nao Wayahudi waliunga mkono mashtaka hayo wakisema kwamba hayo yote yalikuwa kweli.
10 Basi, mkuu wa mkoa alimwashiria Paulo aseme. Naye Paulo akasema, “Nafurahi kujitetea mbele yako nikijua kwamba umekuwa hakimu wa taifa hili kwa miaka mingi.
11 Unaweza kujihakikishia kwamba si zaidi ya siku kumi na mbili tu zimepita tangu nilipokwenda kuabudu Yerusalemu.
12 Wayahudi hawakunikuta nikijadiliana na mtu yeyote. Hawakunikuta nikichochea watu Hekaluni wala katika masunagogi yao, wala mahali pengine popote katika mji huo.
Matendo 24 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 24:8-12 in Biblia ya Kiswahili

8 Ukimwuliza Paulo kuhusu mambo haya, hata utaweza kujifunza ni kitu gani tumemshtakia.”
9 Wayahudi nao wakamshtaki Paulo, wakisema kwamba haya mambo yalikuwa kweli.
10 Liwali alipompungia mkono ili Paulo aongee, Paulo alijibu, “Ninajua ya kwamba kwa miaka mingi umekua mwamuzi wa taifa hili, na nina furaha kujieleza mwenyewe kwako.
11 Waweza kuhakikisha kuwa hazijapita siku zaidi ya kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda kuabudu Yerusalemu.
12 Na waliponikuta katika hekalu, sikubishana na mtu yeyote, na sikufanya fujo katika mkutano, wala katika masinagogi wala ndani ya mji;
Matendo ya Mitume 24 in Biblia ya Kiswahili