Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 24:13-20 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 24:13-20 in Biblia Takatifu

13 Wala hawawezi kuthibitisha mashtaka waliyotoa juu yangu.
14 Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu na wazee wetu nikiishi kufuatana na Njia ile ambayo wao wanaiita chama cha uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya Sheria na manabii.
15 Mimi namtumainia Mungu, na wao wanalo tumaini hilo, kwamba watu, wema na wabaya, watafufuka.
16 Kwa hiyo ninajitahidi daima kuwa na dhamiri njema mbele ya Mungu na mbele ya watu.
17 “Baada ya kukaa mbali kwa miaka kadhaa, nilirudi Yerusalemu ili kuwapelekea wananchi wenzangu msaada na kutoa dhabihu.
18 Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta Hekaluni, nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi la watu wala ghasia.
19 Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia; hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana chochote cha kusema dhidi yangu.
20 Au, waache hawa walio hapa waseme kosa waliloliona kwangu wakati niliposimama mbele ya Baraza lao kuu,
Matendo 24 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 24:13-20 in Biblia ya Kiswahili

13 na wala hawawezi kuhakikisha kwako mashitaka wanayoyashitaki dhidi yangu.
14 Ila nakiri hili kwako, ya kwamba kwa njia ile ambayo wanaiita dhehebu, kwa njia iyo hiyo ninamtumikia Mungu wa baba zetu. Mimi ni mwaminifu kwa yote yaliyoko kwenye sheria na maandiko ya manabii.
15 Nina ujasiri ule ule kwa Mungu ambao hata hao nao wanaungojea, kuja kwa ufufuo wa wafu, kwa wote wenye haki na wasio na haki pia;
16 na kwa hili, ninafanya kazi ili niwe na dhamira isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu kupitia mambo yote.
17 Sasa Baada ya miaka mingi nimekuja kuleta msaada kwa taifa langu na zawadi ya fedha.
18 Nilipofanya hivi, Wayahudi fulani wa Asia wakanikuta ndani ya sherehe ya utakaso ndani ya hekalu, bila kundi la watu wala ghasia.
19 Watu hawa ambao imewapasa kuwapo mbele yako sasa hivi na waseme kile walichonacho juu yangu kama wana neno lo lote.
20 Au watu hawa wenyewe na waseme ni kosa gani waliloliona kwangu niliposimama mbele za baraza la kiyahudi;
Matendo ya Mitume 24 in Biblia ya Kiswahili