Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 24:11-19 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 24:11-19 in Biblia Takatifu

11 Unaweza kujihakikishia kwamba si zaidi ya siku kumi na mbili tu zimepita tangu nilipokwenda kuabudu Yerusalemu.
12 Wayahudi hawakunikuta nikijadiliana na mtu yeyote. Hawakunikuta nikichochea watu Hekaluni wala katika masunagogi yao, wala mahali pengine popote katika mji huo.
13 Wala hawawezi kuthibitisha mashtaka waliyotoa juu yangu.
14 Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu na wazee wetu nikiishi kufuatana na Njia ile ambayo wao wanaiita chama cha uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya Sheria na manabii.
15 Mimi namtumainia Mungu, na wao wanalo tumaini hilo, kwamba watu, wema na wabaya, watafufuka.
16 Kwa hiyo ninajitahidi daima kuwa na dhamiri njema mbele ya Mungu na mbele ya watu.
17 “Baada ya kukaa mbali kwa miaka kadhaa, nilirudi Yerusalemu ili kuwapelekea wananchi wenzangu msaada na kutoa dhabihu.
18 Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta Hekaluni, nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi la watu wala ghasia.
19 Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia; hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana chochote cha kusema dhidi yangu.
Matendo 24 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 24:11-19 in Biblia ya Kiswahili

11 Waweza kuhakikisha kuwa hazijapita siku zaidi ya kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda kuabudu Yerusalemu.
12 Na waliponikuta katika hekalu, sikubishana na mtu yeyote, na sikufanya fujo katika mkutano, wala katika masinagogi wala ndani ya mji;
13 na wala hawawezi kuhakikisha kwako mashitaka wanayoyashitaki dhidi yangu.
14 Ila nakiri hili kwako, ya kwamba kwa njia ile ambayo wanaiita dhehebu, kwa njia iyo hiyo ninamtumikia Mungu wa baba zetu. Mimi ni mwaminifu kwa yote yaliyoko kwenye sheria na maandiko ya manabii.
15 Nina ujasiri ule ule kwa Mungu ambao hata hao nao wanaungojea, kuja kwa ufufuo wa wafu, kwa wote wenye haki na wasio na haki pia;
16 na kwa hili, ninafanya kazi ili niwe na dhamira isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu kupitia mambo yote.
17 Sasa Baada ya miaka mingi nimekuja kuleta msaada kwa taifa langu na zawadi ya fedha.
18 Nilipofanya hivi, Wayahudi fulani wa Asia wakanikuta ndani ya sherehe ya utakaso ndani ya hekalu, bila kundi la watu wala ghasia.
19 Watu hawa ambao imewapasa kuwapo mbele yako sasa hivi na waseme kile walichonacho juu yangu kama wana neno lo lote.
Matendo ya Mitume 24 in Biblia ya Kiswahili