Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 1:18-26 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 1:18-26 in Biblia Takatifu

18 (“Mnajua kwamba yeye alinunua shamba kwa zile fedha alizopata kutokana na kitendo chake kiovu. Akaanguka chini, akapasuka na matumbo yake yakamwagika nje.
19 Kila mtu katika Yerusalemu alisikia habari za tukio hilo na hivyo, kwa lugha yao, wakaliita lile shamba Hekeli Dama, maana yake, Shamba la Damu.)
20 Basi, imeandikwa katika kitabu cha Zaburi: Nyumba yake ibaki mahame; mtu yeyote asiishi ndani yake. Tena imeandikwa: Mtu mwingine achukue nafasi yake katika huduma hiyo.
21 Kwa hiyo, ni lazima mtu mwingine ajiunge nasi kama shahidi wa ufufuo wake Bwana Yesu.
22 Anapaswa kuwa mmoja wa wale waliokuwa katika kundi letu wakati wote Bwana alipokuwa anasafiri pamoja nasi, tangu wakati Yohane alipokuwa anabatiza mpaka siku ile Yesu alipochukuliwa kutoka kwetu kwenda mbinguni.”
23 Basi, wakataja majina ya watu wawili; wa kwanza Yosefu aliyeitwa Barsaba (au pia Yusto), na wa pili Mathia.
24 Kisha wakasali: “Bwana, wewe unajua mioyo ya watu wote. Hivyo, utuonyeshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua
25 ili achukue nafasi hii ya huduma ya kitume aliyoacha Yuda akaenda mahali pake mwenyewe.”
26 Hapo, wakapiga kura; kura ikampata Mathia, naye akaongezwa katika idadi ya wale mitume wengine kumi na mmoja.
Matendo 1 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 1:18-26 in Biblia ya Kiswahili

18 (Sasa mtu huyu alinunua eneo kwa kile alichokipokea kwa uovu wake na hapo alianguka akitanguliza kichwa, mwili ukapasuka na matumbo yake yote yakawa wazi yakamwagika.
19 Wote walioishi Yerusalemu walisikia kuhusu hili, hivyo eneo hilo wakaliita kwa lugha yao “Akeldama” hilo ni “shamba la damu.”)
20 “Kwenye kitabu cha Zaburi imeandikwa, 'Ngoja eneo lake liwe hame na isiruhusiwe hata mmoja kuishi pale;' na, 'Ruhusu mtu mwingine achukue nafasi yake ya uongozi.'
21 Hiyo ni muhimu, kwa hiyo, mmoja wa wanaume ambao waliambatana nasi wakati Bwana Yesu alipotoka na kuingia kati yetu,
22 kuanzia kwenye ubatizo wa Yohana mpaka siku ile alipotwaliwa juu, lazima awe shahidi wa ufufuo pamoja nasi.
23 “Wakaweka mbele wanaume wawili, Yusufu aitwaye Barnaba, ambaye pia aliitwa Yusto na Mathia.
24 Wao waliomba wakisema, “Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, hivyo weka wazi yupi kati ya wawili hawa ambaye umemchagua
25 kuchukua nafasi katika huduma na utume, ambapo Yuda alitenda uovu na kwenda mahali pake.”
26 Wakapiga kura kwa ajili yao, na kura ikamwangukia Mathia ambaye alihesabiwa pamoja na wale mitume kumi na moja.
Matendo ya Mitume 1 in Biblia ya Kiswahili