Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 16:1-10 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 16:1-10 in Biblia Takatifu

1 Paulo alifika Derbe na Lustra, ambako aliishi mfuasi mmoja aitwaye Timotheo. Mama yake ambaye pia alikuwa mfuasi, alikuwa Myahudi; lakini baba yake alikuwa Mgiriki.
2 Timotheo alikuwa na sifa kubwa kati ya wale ndugu wa Lustra na Ikonio.
3 Paulo alitaka Timotheo aandamane naye safarini, kwa hiyo alimtahiri. Alifanya hivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishi sehemu hizo walijua kwamba baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.
4 Walipokuwa wanapita katika ile miji waliwapa watu yale maagizo yaliyotolewa na mitume na wazee kule Yerusalemu, wakawaambia wayazingatie.
5 Hivyo, yale makanisa yalizidi kuwa imara katika imani, na idadi ya waumini ikaongezeka kila siku.
6 Walipitia sehemu za Frugia na Galatia kwani Roho Mtakatifu hakuwaruhusu kuhubiri huo ujumbe mkoani Asia.
7 Walipofika kwenye mipaka ya Musia, walijaribu kuingia mkoani Bithunia, lakini Roho wa Yesu hakuwaruhusu.
8 Basi, walipitia Musia, wakaenda moja kwa moja mpaka Troa.
9 Usiku huo, Paulo aliona ono ambalo alimwona mtu mmoja wa Makedonia amesimama pale na kumwomba: “Vuka, uje Makedonia ukatusaidie.”
10 Mara baada ya Paulo kuona ono hilo, tulijitayarisha kwenda Makedonia bila kukawia, tukiwa na hakika kwamba Mungu ametuita tuwapelekee Habari Njema.
Matendo 16 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 16:1-10 in Biblia ya Kiswahili

1 Paulo pia alipokuja Derbe na Lystra; na tazama, pale palikuwepo na mwanafunzi aitwaye Timotheo, ni Kijana aliyezaliwa na mama wa Kiyahudi ambaye ni muumini na baba yake ni Mgiriki.
2 Watu wa Listra na Ikonia walimshudia vizuri.
3 Paulo alimtaka ili asafiri naye, hivyo akamchukua na kumtahiri kwa sababu ya Wayahudi waliokuwako huko kwani wote walimjua kuwa baba yake ni Mgiriki.
4 Walipokuwa wakienda walipita kwenye miji na kutoa maagizo kwa makanisa ili kuyatii maagizo hayo yaliandikwa na mitume na wazee huko Yerusalemu.
5 Hivyo makanisa yakaimarishwa katika imani na walioamini wakaongezeka kwa idadi kila siku.
6 Paulo na mwenzake wakaenda Firigia na Galatia, kwani Roho wa Mungu aliwakataza kuhubiri neno huko kwenye jimbo la Asia.
7 Walipokaribia Misia, walijaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu akawakataza.
8 Kwa hiyo wakapita Misia wakaja mpaka Mji wa Troa.
9 Maono yalimtokea Paulo usiku, kulikuwa na mtu wa Makedonia amesimama, akimwita na kusema “Njoni mtusaidie huku Makedonia”.
10 Paulo alipoona maono, mara tukajiandaa kwenda Makedonia, akijua kwamba Mungu alituita kwenda kuwahubiria injili.
Matendo ya Mitume 16 in Biblia ya Kiswahili