Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 12:8-19 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 12:8-19 in Biblia Takatifu

8 Malaika akamwambia, “Jifunge mshipi wako, vaa viatu vyako.” Akafanya hivyo. Kisha huyo malaika akamwambia, “Vaa koti lako, unifuate.”
9 Petro akamfuata nje lakini hakujua kama hayo yaliyofanywa na huyo malaika yalikuwa ya kweli; alidhani alikuwa anaota ndoto.
10 Walipita kituo cha kwanza cha ulinzi na cha pili, halafu wakafika kwenye mlango wa chuma wa kuingilia mjini. Huo mlango ukawafungukia wenyewe, nao wakatoka nje. Wakawa wanatembea katika barabara moja na mara yule malaika akamwacha Petro peke yake.
11 Hapo ndipo Petro alipotambua yaliyotukia, akasema, “Sasa najua kwa hakika kwamba Bwana amemtuma malaika wake akaniokoa kutoka katika mkono wa Herode na kutoka katika mambo yale yote watu wa Israeli waliyotazamia.”
12 Alipotambua hivyo alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Maria mama yake Yohane aitwaye Marko. Humo watu wengi walikuwa wamekusanyika wakisali.
13 Petro alibisha mlango wa nje na mtumishi mmoja msichana aitwaye Roda, akaenda mlangoni kuitikia.
14 Huyo msichana aliitambua sauti ya Petro akafurahi mno, hata badala ya kuufungua ule mlango, akakimbilia ndani na kuwaambia kwamba Petro alikuwa amesimama nje mlangoni.
15 Wakamwambia yule msichana, “Una wazimu!” Lakini yeye akasisitiza kwamba ilikuwa kweli. Nao wakamwambia, “Huyo ni malaika wake.”
16 Wakati huo Petro alikuwa anaendelea kupiga hodi. Mwishowe walifungua mlango, wakamwona, wakashangaa.
17 Petro aliwaashiria kwa mkono wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Kisha akawaambia watoe taarifa ya jambo hilo kwa Yakobo na wale ndugu wengine, halafu akatoka akaenda mahali pengine.
18 Kulipokucha, ulitokea wasiwasi mkubwa kati ya wale askari kuhusu yaliyokuwa yamempata Petro.
19 Herode aliamuru ufanywe msako lakini hawakuweza kumpata. Hivyo aliamuru wale askari wahojiwe, akatoa amri wauawe. Halafu akatoka huko Yudea akaenda Kaisarea ambako alikaa.
Matendo 12 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 12:8-19 in Biblia ya Kiswahili

8 Malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na vaa viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Malaika akamwambia, “Vaa vazi lako na unifuate.”
9 Hivyo Petro akamfuata Malaika na akatoka nje. Hakuamini kilichofanywa na malaika kama ni cha kweli. Alidhani anaona maono.
10 Baada ya kupita lindo la kwanza na la pili, wakafika kwenye geti la chuma la kuingilia kwenda mjini, likafunguka lenyewe kwa ajili yao. Wakatoka nje wakashuka kwenye mtaa, mara Malaika akamwacha.
11 Petro alipojitambua, akasema, “Sasa nimeamini kuwa Bwana alimtuma Malaika wake ili kunitoa katika mikono ya Herode, na kwa matarajio ya watu wote wa uyahudi.”
12 Baada ya kujua haya, akaja kwenye nyumba ya Mariamu mama yake Yohana ambaye ni Marko; Wakristo wengi walikusanyika wakiomba.
13 Alipobisha kwenye mlango wa kizuizi, mtumishi mmoja msichana anayeitwa Roda akaja kufungua.
14 Alipotambua ni sauti ya Petro, kwa furaha akashindwa kuufungua mlango; badala yake, akakimbia ndani ya chumba; na kuwajulisha kuwa Petro amesimama mbele ya Mlango.
15 Hivyo, Wakasema kwake, “Wewe ni mwendawazimu” lakini alikazia kuwa ni kweli ni yeye. Wakasema “Huyo ni malaika wake.”
16 Lakini Petro aliendelea kubisha, na walipofungua mlango, wakamwona na wakashangaa sana. Petro akawanyamazisha kwa mkono kimya kimya na akawaambia jinsi Bwana alivyomtoa kutoka Gerezani. akasema,
17 “Wajulishe haya mambo Yakobo na ndugu zake.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.
18 Kulipokuwa mchana, kukawa na huzuni kubwa kati ya askari, kuhusiana na kilichotokea kwa Petro.
19 Baada ya Herode kumtafuta na hakumwona akawauliza walinzi na akaamuru wauawe. Akaenda kutoka uyahudi mpaka Kaisaria na kukaa huko.
Matendo ya Mitume 12 in Biblia ya Kiswahili