22 Wakasema, “Akida mmoja jina lake Kornelio, mtu wa haki na hupenda kumwabudu Mungu, na watu humsema vyema katika taifa lote la kiyahudi, ameambiwa na malaika wa Mungu kukutuma ili kwenda kwenye nyumba yake, ili asikie ujumbe kutoka kwako.”
23 Petro akawakaribisha kuingia ndani na kukaa pamoja naye. Asubuhi iliyofuata akaamka akaenda pamoja naye, na ndugu wachache kutoka Yafa wakaambatana naye.
24 Siku iliyofuata walikuja Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwasubiri; na alikuwa amewaita pamoja ndugu zake na marafiki zake wa karibu.
25 Wakati Petro akiingia ndani, Kornelio akamlaki na kuinama hadi chini kwenye miguu yake kwa kumheshimu.
26 Lakini Petro akamwinua na kusema “Simama; mimi mwenyewe pia ni mwanadamu.”
27 Wakati Petro akiwa anaongea naye, alienda ndani akakuta watu wamekusanyika pamoja.
28 Akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua kuwa siyo sheria ya kiyahudi kushirikiana au kutembelewa na mtu ambaye si wa taifa hili. Lakini Mungu amenionesha mimi kuwa sipaswi kumwita mtu yeyote ni najisi au mchafu.
29 Na ndiyo maana nimekuja bila kubisha, nilipotumwa kwa ajili ya hiyo. Kwa hiyo niwaulize kwa nini mlitumwa kwa ajili yangu.”
30 Kornelio akasema, “Siku nne zilizopita, wakati kama huu nilikuwa naomba muda wa saa tisa mchana ndani ya nyumba yangu; Nikaona mbele yangu mtu amesimama akiwa na mavazi meupe,
31 Akaniambia “Kornelio maombi yako yamesikiwa na Mungu, na zawadi zako kwa masikini zimekuwa ukumbusho mbele za Mungu.
32 Kwa hiyo tuma mtu Yafa na akamwite mtu mmoja anayeitwa Simoni aje kwako, ambaye pia huitwa Petro. ambaye anaishi kwa mtengenezaji wa Ngozi mmoja aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko pembeni mwa bahari.
33 Zingatia: Msatri huu, “Naya atakapokuja atasema nanyi,” haumo kwenye maandiko ya kale.
34 Ndipo Petro akafungua mdomo wake na kusema “Kweli, nimeamini kuwa Mungu hawezi kuwa na upendeleo.
35 Badala yake, kila taifa mtu yeyote anayemwabudu na kufanya matendo ya haki anakubalika kwake.
36 Unajua ujumbe alioutoa kwa watu wa Israel, alipokuwa akitangaza habari njema ya amani kupitia Yesu Kristo ambaye ni Bwana wa wote-
37 ninyi wenyewe mnajua tukio lililotokea, ambalo limetokea Yudea yote na lilianzia Galilaya, baada ya ubatizo ambao Yohana alitangaza.
38 tukio lililokuwa linamhusu Yesu Kristo jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu. Alienda akifanya mema na kuponya wote walioteswa na ibilsi, kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja naye.
39 Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika nchi za Uyahudi na katika Yerusalemu- huyu ni Yesu waliyemuua na kumtundika mtini.
40 Huyu mtu Mungu alimfufua siku ya tatu na kumpa kujulikana,
41 si kwa watu wote, lakini kwa mashahidi waliochaguliwa kabla na Mungu. - sisi wenyewe, tulio kula naye na kunywa naye baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.
42 Ametuagiza kuhubiri kwa watu na kushuhudia kuwa huyu ndiye ambaye Mungu alimchagua kuwa mwamuzi wa walio hai na waliokufa.
43 Katika yeye manabii wote washuhudie, ili kwamba kila anayeamini katika yeye atapokea msamaha wa dhambi kupitia jina lake.”
44 Wakati Petro akiendelea kusema haya, Roho Mtakatifu akawajaza wote waliokuwa wakisikiliza ujumbe wake.