Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Marko 9:37-45 in Swahili (individual language)

Help us?

Marko 9:37-45 in Biblia Takatifu

37 “Anayempokea mtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule aliyenituma.”
38 Yohane akamwambia, “Mwalimu, tumemwona mtu mmoja akitoa pepo kwa kulitumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa yeye si mmoja wetu.”
39 Lakini Yesu akasema, “Msimkataze, maana hakuna mtu anayefanya muujiza kwa jina langu, na papo hapo akaweza kusema mabaya juu yangu.
40 Maana, asiyepingana nasi, yuko upande wetu.
41 Mtu yeyote atakeyewapeni kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu ninyi ni watu wake Kristo, hakika hatakosa kupata tuzo lake.
42 “Mtu yeyote atakayemfanya mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini atende dhambi, ingekuwa afadhali kwa mtu huyo kufungiwa shingoni mwake jiwe kubwa la kusagia na kutupwa baharini.
43 Mkono wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia kwenye uzima bila mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu.
44 Humo, wadudu wake hawafi na moto hauzimiki.
45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uzima bila mguu mmoja, kuliko kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
Marko 9 in Biblia Takatifu

Marko 9:37-45 in Biblia ya Kiswahili

37 “Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.”
38 Yohana alimwambia, “Mwalimu tulimwona mtu anatoa pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu hatufuati.”
39 Lakini Yesu alisema, “Msimzuie, kwa kuwa hakuna atakayefanya kazi kubwa kwa jina langu na ndipo baadaye aseme neno baya lolote juu yangu.
40 Yeyote asiyekuwa kinyume nasi yuko upande wetu.
41 Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo, kweli nawaambia, hatapoteza thawabu yake.
42 Yeyote anayewakosesha hawa wadogo waniaminio mimi, ingekuwa vyema kwake kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini.
43 Kama mkono wako ukikukosesha ukate. Ni heri kuingia katika uzima bila mkono kuliko kuingia kwenye hukumu ukiwa na mikono yote. Katika moto “usiozimika”.
44 (Zingatia: Mstari hii, “Mahali ambapo funza hawafi na moto usiozimika.” haumo katika nakala za kale).
45 Kama mguu wako ukikukosesha, ukate. Ni vyema kwako kuingia uzimani ukiwa kilema, kuliko kutupwa hukumuni na miguu miwili.
Marko 9 in Biblia ya Kiswahili