Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Marko 5:5-26 in Swahili (individual language)

Help us?

Marko 5:5-26 in Biblia Takatifu

5 Mchana na usiku alikaa makaburini na milimani akipaaza sauti na kujikatakata kwa mawe.
6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia, akamwinamia
7 akisema kwa sauti kubwa, “Una shauri gani nami, wewe Yesu Mwana wa Mungu aliye juu? Kwa jina la Mungu, nakusihi usinitese!”
8 (Alisema hivyo kwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia, “Pepo mchafu, mtoke mtu huyu.”)
9 Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Naye akajibu, “Jina langu ni Jeshi, maana sisi tu wengi.”
10 Kisha akamsihi Yesu asiwafukuze hao pepo katika nchi ile.
11 Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe malishoni kwenye mteremko wa mlima.
12 Basi, hao pepo wakamsihi, “Utupeleke kwa hao nguruwe, tuwaingie.”
13 Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka, wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe wapatao elfu mbili likaporomoka kwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani, likatumbukia majini.
14 Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilo mjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliyotukia.
15 Wakamwendea Yesu, wakamwona na mtu yuleyule aliyekuwa amepagawa na jeshi la pepo ameketi chini, amevaa nguo na ana akili yake sawa, wakaogopa.
16 Watu walishuhudia tukio hilo wakaeleza wengine mambo yaliyompata huyo mtu aliyekuwa amepagawa na pepo na juu ya wale nguruwe.
17 Basi, wakaanza kumwomba aondoke katika nchi yao.
18 Yesu alipokuwa anapanda mashuani, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo akamwomba amruhusu kwenda naye.
19 Lakini Yesu akamkatalia. Badala yake akamwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako, ukawaambie mambo yote Bwana aliyokutendea na jinsi alivyokuonea huruma.”
20 Basi, huyo mtu akaenda, akaanza kutangaza huko Dekapoli mambo yote Yesu aliyomtendea; watu wote wakashangaa.
21 Yesu alivukia tena upande wa pili wa ziwa kwa mashua. Umati mkubwa wa watu ukakusanyika mbele yake, naye akawa amesimama kando ya ziwa.
22 Hapo akaja mmojawapo wa maofisa wa sunagogi, jina lake Yairo. Alipomwona Yesu, akajitupa mbele ya miguu yake,
23 akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa karibu kufa. Twende tafadhali, ukamwekee mikono yako, apate kupona na kuishi.”
24 Basi, Yesu akaondoka pamoja naye. Watu wengi sana wakamfuata, wakawa wanamsonga kila upande.
25 Mmojawapo alikuwa mwanamke mwenye ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili.
26 Mwanamke huyo alikuwa amekwisha sumbuka sana kuwaendea waganga wengi. Na ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote, hakupata nafuu bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.
Marko 5 in Biblia Takatifu

Marko 5:5-26 in Biblia ya Kiswahili

5 Usiku na mchana akiwa makaburini na milimani, alilia na kujikata yeye mwenyewe kwa mawe makali.
6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alikimbilia kwake na kuinama mbele yake.
7 Alilia kwa sauti kuu, “Wataka nikufanyie nini, Yesu, Mwana wa Mungu aliye Juu sana? Ninakusihi kwa Mungu mwenyewe, usinitese.”
8 Kwa kuwa alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe roho mchafu.”
9 Naye alimwuliza, “Jina lako ni nani?” Naye alimjibu, “Jina langu ni Legion, kwa kuwa tuko wengi.”
10 Alimsihi tena na tena asiwapeleke nje ya mkoa.
11 Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likilishwa juu ya kilima,
12 nao walimsihi, wakisema, “Tutume kwa nguruwe; tuingie ndani yao.”
13 Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu waliwatoka na kuingia ndani ya nguruwe, nao walikimbilia chini ya kilima mpaka baharini, na karibia nguruwe elfu mbili walizama baharini.
14 Na wale waliokuwa wakiwalisha nguruwe walikimbia na kutoa taarifa ya kilichotokea katika mji na katika nchi. Ndipo watu wengi walitoka kwenda kuona kilichotokea.
15 Ndipo walikuja kwa Yesu na walimwona mtu aliyepagawa na pepo—aliyekuwa na Jeshi—amekaa chini, amevikwa, na akiwa katika akili yake timamu, nao waliogopa.
16 Wale waliokuwa wameona kilichotokea kwa mtu aliyekuwa amepagawa na pepo waliwaambia kilichotokea kwake na pia kuhusu nguruwe.
17 Nao walianza kumsihi aondoke katika mkoa wao.
18 Na alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo alimsihi kwamba aende pamoja naye.
19 Lakini hakumruhusu, lakini alimwambia, “Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako, na uwaambie alikufanyia Bwana, na rehema aliyokupa.”
20 Hivyo alienda na alianza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake katika Dekapoli, na kila mmoja alistaajabu.
21 Na wakati Yesu alipovuka tena upande mwingine, ndani ya mtumbwi, umati mkubwa ulikusanyika kumzunguka, alipokuwa kando ya bahari.
22 Na mmoja wa kiongozi wa sinagogi, aliyeitwa Yairo, alikuja, na alipomwona, alianguka miguuni pake.
23 Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, “Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili kwamba aweze kupata afya na kuishi.”
24 Hivyo alikwenda pamoja naye, na umati mkubwa ulimfuata nao walimzonga karibu wakimzunguka.
25 Kulikuwa na mwanamke ambaye damu yake ilikuwa imetoka kwa miaka kumi na miwili.
26 Aliteseka vya kutosha chini ya matabibu wengi na alitumia kila kitu alichokuwa nacho. Hata hivyo hakusaidika kwa chochote, lakini badala yake alizidi kuwa na hali mbaya.
Marko 5 in Biblia ya Kiswahili