24 Akawaambia, “Iweni makini kwa kile mnachokisikia, kwa kuwa kipimo mpimacho, ndicho mtakachopimiwa, na itaongezwa kwenu.
25 Kwa sababu yeye aliyenacho, atapokea zaidi, na yule asiyenacho, kutoka kwake vitachukuliwa hata vile alivyonavyo.”
26 Na akasema, “Ufalme wa Mungu umefananishwa na mtu aliyepanda mbegu katika udongo.
27 Alipolala usiku na kuamka asubuhi, na mbegu zikachipuka na kukua, ingawa hajui ilivyotokea.
28 Dunia hutoa mbegu yenyewe; kwanza majani, halafu maua, halafu mbegu zilizo komaa.
29 Na wakati mbegu itakapokua imeiva mara hupeleka mundu, kwa sababu mavuno yamewadia.”
30 Na akasema, “tuufananishe ufalme wa Mungu na kitu gani, au tutumie mfano gani kuuelezea?.