Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 8

Mambo ya Walawi 8:27-30

Help us?
Click on verse(s) to share them!
27Akaiweka yote mikoni mwa Aroni na katika mikono ya wanawe na kuitikisa mbele za Yahweh kuwa sadaka ya kutikiswa
28Kisha Musa akaichukua mikate hiyo kutoka mikononi mwao na kuiteketeza juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Zilikuwa ni sadaka ya kuwekwa wakfu na ilitoa harufu ya kupendeza. Ilikuwa sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto.
29Musa akakichukua kidari na kukitikisa kuwa sadaka ya kutikiswa kwa Yahweh. Ilikuwa ni mgao wa Musa wa kondoo wa kuwekewa mikono kwa makuhani, Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru yeye.
30Musa akatwaa sehemu ya mafuta ya upako na damu iliyokuwa juu ya madhabahu; naye akayanyunyiza haya juu ya nguo za Aroni, juu ya nguo zake mwenyewe na juu ya nguo za wana wa Aruni waliokua pamoja naye. Kwa njia hii alimtenga Aroni na nguo zake, na wanawe na nguo zao kwa ajili ya Yahweh.

Read Mambo ya Walawi 8Mambo ya Walawi 8
Compare Mambo ya Walawi 8:27-30Mambo ya Walawi 8:27-30