Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 5

Mambo ya Walawi 5:11-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11Lakini kama hataweza kununua hua wawili au makinda ya njiwa mawili, ndipo ataleta kama dhabihu ya dhambi zake sehemu ya kumi ya unga laini kama sadaka ya dhambi. Asiweke mafuta wala ubani juu yake, kwa kuwa ni sadaka ya dhambi.
12Atauleta kwa kuhani, na kuhani atachukua konzi moja ya unga kama ukumbusho wa wema wa Bwana na atauweka juu ya madhabahu na kuteketeza juu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
13Kuhani atafanya upatanisho kwa dhambi yoyote aliyofanya mtu yeyote, mtu huyo atasamehewa. Na sadaka inayobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyo sadaka ya nafaka.'”
14Bwana akamwambia Musa, akasema,
15“Kama mtu akikiuka amri na kufanya dhambi kinyume na mambo matakatifu ya Bwana, lakini akifanya bila kukusudia ataleta sadaka ya hatia kwa Bwana. Sadaka hii itakuwa ni kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi; thamani yake halisi kifedha kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kama sadaka ya hatia.
16Lazima atalipa kwa Bwana kwa kile alichokosa kulingana na kitakatifu, na ataongezea moja ya tano na kumpa kuhani. Ndipo kuhani ataweka upatanisho kwa ajili yake pamoja na kondoo wa sadaka ya hatia, na mtu atakuwa amesamehewa.

Read Mambo ya Walawi 5Mambo ya Walawi 5
Compare Mambo ya Walawi 5:11-16Mambo ya Walawi 5:11-16