Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 25

Mambo ya Walawi 25:10-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
10Nanyi mtautenga mwaka wa hamsini kwa ajili ya Yahweh na mtatangaza uhuru katika nchi yote kwa wakazi wote. Kutakuwa na Yubile kwa ajili yenu, ambayo kwayo mali na watumwa ni lazima warejeshwe kwa familia zao.
11Mwaka wa saba kutakuwa na Yubile kwenu. Hamtapanda wala kusimamia mavuno ya kijioteshacho chenyewe, na kukusanya kichipukacho kwenye mizabibu isiyokatiwa matawi.
12Kwa sababu hiyo ni Yubile takatifu kwenu. Nanyi mtakula mazao yanayokua yenyewe kutoka mashambani.
13Ni lazima muwarejeshe kila mmoja kwenye miliki yake katika mwaka huu wa Yubile.
14Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni shrti msipunjane au kutendeana kwa hila.
15Iwapo unanunua ardhi kutoka kwa jirani yako, zingatia idadi ya miaka na mazao ambayo yaweza kuvunwa mpaka mwaka wa Yubile nyingine. Jirani yako anayeuza ardhi ni lazima aihesabu miaka hiyo pia.
16Miaka inapoongezeka mpaka Yubile nyingine, ataongeza thamani ya ardhi, na miaka inapokuwa michache kufikia Yubile nyingine atashusha thamani, kwa sababu idadi ya mavuno inahusiana na idadi ya miaka kabla ya Yubile nyingine.
17Msipunjane au kutendeana kwa hila, badala yake, yawapasa kumheshi Yahweh Mungu wenu.
18Kwa hiyo basi, ni lazima muyatii maagiza, kuzitunza sheria zangu na kuzitekeleza. Nanyi mtaishi katika nchi katika usalama.
19Nayo nchi itawapa mavuno yake, nanyi mtakula matunda yenu na mtaishi humo salama.
20Labda mtasema, Tutakula nini katika mwaka wa saba? Tazama, hatuwezi kupanda wala kukusanya mazao yetu.”
21Nitaiamru baraaka yangu ije juu yenu katika mwaka wa sita, nayo itatoa mavuno ya kutosha kwa miaka mitatu.
22Mtapanda katika mwaka wa nane na mtaendelea kula mazao ya miaka iliyopita na kutoka kwenye ghala la chakula. Mpaka mavuno ya mwaka wa tisa yatakapofika, mtaweza kula kutoka kwenye riziki iliyohifadhiwa katika miaka iliyopita
23Ardhi haitauzwa kwa mmiliki mpya wa kudumu, kwa sababu ardhi ni mali yangu. Ninyi nyote mu wageni na wakazi wa muda juu ya ardhi yangu.
24Ni lazima muitunze haki ya ukombozi kwa ajili ya ardhi yote mtakayoimiliki; itawapasa kuruhusu ardhi inunuliwe tena na familia ambayo wewe uliinunua hiyo ardhi kutoka kwao.

Read Mambo ya Walawi 25Mambo ya Walawi 25
Compare Mambo ya Walawi 25:10-24Mambo ya Walawi 25:10-24