Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 24

Mambo ya Walawi 24:2-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2“Waamru watu wa Israeli wakuletee mafuta halisi yaliyokamliwa kutokana na mizeituni ili yatumike kwenye taa, ili kwamba taa ziweze kuwaka daima na kuleta mwanga.
3Nje ya pazia lililoko mbele ya sanduku la maamzi ndani ya hema la kukutania, Aroni ataiwasha daima taa mbele za Yahweh, tangu asubuhi hata jioni. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu.
4Kuhani mkuu atazifanya taa ziwake daima mbele za Yahweh, taa hizo zilizo kwenye kinara cha dhahabu safi.
5Yawapasa kuchukua unga laini na kuoka kwa huo mikate kumi na miwili. Ni lazima kuwe na mbili za kumi za efa za unga katika kila mkate.
6Kisha mtaipanga juu ya meza ya dhahabu safi mbele za Yahweh katika safu mbili, mikate sita katika kila safu,
7Mtaweka uvumba safi kando ya kila safu ya mikata kuwa sadaka ya kuwakilisha. Uvumba huo utachomwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh.
8Kila siku ya Sabato kuhani mkuu sharti aipange kwa utaratibu hiyo mikate mbele za Yahweh kwa niaba ya watu wa Israeli, iwe ishara ya agano la milele.
9Sadaka hii itakuwa kwa ajili ya Aroni na wanawe, na ni lazima waile mahali palipo patakatifu, kwa kuwa ni sehemu ya matoleo kwa Yahweh yaliyofanywa kwa moto.”
10Sasa ilitokea kwamba mwana wa mwanamke Mwisraeli, ambaye baba yake alikuwa Mmisri, alikwenda miongoni mwa watu wa Israeli. Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akagombana na mwanume Mwisraeli kambini.
11Mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru jina la Yahweh na kumlaani Mungu, kwa hiyo watu wakamleta kwa Musa. Jina la mama yake aliitwa Shelomithi, binti wa Dibri, kutoka kabila la Dani.
12Wakamweka kizuizini mpaka Yahweh mwenyewe atakapotangaza mapenzi yake kwao.

Read Mambo ya Walawi 24Mambo ya Walawi 24
Compare Mambo ya Walawi 24:2-12Mambo ya Walawi 24:2-12