Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 20

Mambo ya Walawi 20:17-22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
17Ikiwa mwanaume analala na dada yake, ama ni binti ya baba yake au binti ya mama yake—ikiwa wamelala pamoja, hilo ni jambo la aibu. Ni lazima wakatiliwe mbali watoke machoni pa watu wao, kwa sababu amelala na dada yake. Ni lazima aibebe hatia yake.
18Kama mwanaume analala na mwanamke katika kipindi cha hedhi yake, na amekutana naye kimwili, atakuwa amefunua mtiririko wa damu yake, chanzo cha damu yake. Ni lizima wote wawili wakatiliwe mbali kutoka mingoni mwa watu wao.
19Usilale na dada ya mama yako, au dada ya baba yako, kwa sababu ungeweza kumwaibisha jamaa yako wa karibu. Ni lazima utabeba hatia yako mwenyewe.
20Ikiwa mwanaume analala na shangazi yake, atakuwa amemfedhehesha mjomba wake. Wanapokufa, nitawaadhibu wote wawili, na wanapokufa nitauondolea mbali urithi wa watoto wao ambao wangeliupokea kutoka kwa wazazi wao.
21Ikiwa mwanaume anamwoa mke wa kaka yake wakati ambapo kaka yake angali hai, hilo ni jambo la aibu. Amemfedhehesha kaka yake, na nitaondolea mbali mali yoyote amabayo watoto wao wangerithi kutoka kwa wazazi wao.
22Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri na sheria zangu zote; ni lazima mzitii ili kwamba ile nchi ambayo ninawaleta kuishi isiwatapike nyinyi.

Read Mambo ya Walawi 20Mambo ya Walawi 20
Compare Mambo ya Walawi 20:17-22Mambo ya Walawi 20:17-22