Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 15

Mambo ya Walawi 15:14-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
14Katika siku ya nane lazima achukue njiwa wawili au kinda mbili za njiwa na aje mbele za Yahwe pakuingilia kwenye hema ya mkutano; pale lazima atoe hao ndege kwa kuhani.
15Lazima kuhani awatoe, moja kama sadaka ya dhambi na nyingine kama ya kuteketezwa, na kuhani lazima afanye upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe kwaajili ya kisonono chake.
16Kama mtu yeyote ametokwa na shahawa, ndipo lazima aoge mwili wake wote katika maji; atanajisika mpaka jioni.
17Kila vazi au ngozi ambayo juu yake kuna shahawa lazama paoshwe kwa maji; itakuwa najisi mpaka jioni.
18Na kama mwanamke na mwanaume watalala pamoja na kunakutokwa kwa shahawa kwenda kwa mwanamke, lazima wote wawili waoge katika maji; watakuwa najisi mpaka jioni.
19Mwanamke anapokuwa kwenye hedhi, ataendelea kunajisika kwa siku saba, na yeyote anayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
20Chochote anacholala juu yake wakati wa hedhi kitakuwa najisi; kila kitu ambacho anakalia kitakuwa pia najisi.
21Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
22Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.
23Iwe juu ya kitanda au kitu chochote juu ya popote atakapokaa, kama akikigusa, mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
24Kama mwanaume yeyote akilala naye, na unajisi wa mwanamke ukamgusa, atakuwa amenajisika siku saba. Kila kitanda ambacho anakilalia mwanaume huyo kitanajisika.

Read Mambo ya Walawi 15Mambo ya Walawi 15
Compare Mambo ya Walawi 15:14-24Mambo ya Walawi 15:14-24