Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 7:8-47 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 7:8-47 in Biblia Takatifu

8 Mimi pia ni mtu niliye chini ya mamlaka, na ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, Nenda!, naye huenda; namwambia mwingine, Njoo! naye huja; na nikimwambia mtumishi wangu, Fanya hiki!, hufanya.”
9 Yesu aliposikia hayo, alishangaa; halafu akauelekea ule umati wa watu uliokuwa unamfuata, akasema, “Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli.”
10 Wale watu walipowasili nyumbani walimkuta yule mtumishi hajambo kabisa.
11 Baadaye kidogo Yesu alikwenda katika mji mmoja uitwao Naini, na wafuasi wake pamoja na kundi kubwa la watu waliandamana naye.
12 Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya kijana mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.
13 Bwana alipomwona mama huyo, alimwonea huruma, akamwambia, “Usilie.”
14 Kisha akaenda, akaligusa lile jeneza, na wale waliokuwa wanalichukua wakasimama. Halafu akasema, “Kijana! Nakuamuru, amka!”
15 Yule aliyekufa akaketi, akaanza kuongea. Na Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
16 Watu wote walishikwa na hofu, wakawa wanamtukuza Mungu wakisema: “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”
17 Habari hizo zikaenea kote katika Uyahudi na katika nchi za jirani.
18 Wanafunzi wa Yohane walimpa habari Yohane juu ya mambo hayo yote. Naye Yohane, baada ya kuwaita wawili kati ya wanafunzi wake,
19 aliwatuma kwa Bwana wamwulize: “Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”
20 Wale wanafunzi walipomfikia Yesu wakamwambia, “Yohane Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”
21 Wakati huohuo, Yesu alikuwa anawaponya watu wengi waliokuwa wanateseka kwa magonjwa na waliopagawa na pepo wabaya, akawawezesha vipofu wengi kuona tena.
22 Basi, Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane yale mliyojionea na kuyasikia: vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari njema.
23 Heri mtu yule ambaye hana mashaka nami!”
24 Hapo wajumbe wa Yohane walipokwisha kwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane: “Mlikwenda kule jangwani, hivi mlitaka kuona kitu gani? Mlitaka kuona unyasi unaotikiswa na upepo?
25 Basi, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona mtu aliyevalia mavazi maridadi? La hasha! Wanaovaa mavazi maridadi na kuishi maisha ya anasa, hukaa katika majumba ya wafalme!
26 Basi, niambieni, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, hakika ni zaidi ya nabii.
27 Huyu Yohane ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu: Hapa ni mtumishi wangu, asema Bwana; ninamtuma akutangulie, akutayarishie njia.”
28 Yesu akamalizia kwa kusema, “Nawaambieni, kati ya binadamu wote hakuna aliye mkubwa zaidi kuliko Yohane Mbatizaji. Hata hivyo, yule aliye mdogo kabisa katika ufalme wa Mungu ni mkubwa zaidi kuliko yeye.”
29 Waliposikia hayo watu wote na watoza ushuru waliusifu wema wa Mungu; hao ndio wale waliokuwa wameupokea ubatizo wa Yohane.
30 Lakini Mafarisayo na walimu wa Sheria walikataa mpango wa Mungu uliowahusu wakakataa kubatizwa na Yohane.
31 Yesu akaendelea kusema, “Basi, nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani?
32 Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine: Tumewapigieni ngoma, lakini hamkucheza! Tumeomboleza, lakini hamkulia!
33 Kwa maana Yohane alikuja, yeye alifunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: Amepagawa na pepo!
34 Akaja Mwana wa Mtu; anakula na kunywa, mkasema: Mwangalieni mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi!
35 Hata hivyo, hekima ya Mungu imethibitishwa kuwa njema na wote wale wanaoikubali.”
36 Mfarisayo mmoja alimwalika Yesu kula chakula nyumbani kwake. Akaingia nyumbani mwa huyo Mfarisayo, akakaa kula chakula.
37 Basi, katika mji ule kulikuwa na mama mmoja aliyekuwa anaishi maisha mabaya. Alipopata habari kwamba Yesu yuko nyumbani kwa huyo Mfarisayo, alichukua chupa ya alabasta yenye marashi.
38 Akaja, akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia, na machozi yake yakamdondokea Yesu miguuni. Huyo mwanamke akaipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zake. Kisha akaibusu na kuipaka yale marashi.
39 Yule Mfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo, akawaza moyoni mwake, “Kama mtu huyu angekuwa kweli nabii angejua huyu mwanamke ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.”
40 Yesu akamwambia huyo Mfarisayo, “Simoni, ninacho kitu cha kukwambia.” Naye Simoni akamwambia, “Ndio Mwalimu, sema.” Yesu akasema,
41 “Watu wawili walikuwa wamemkopa mtu fedha: mmoja alikuwa amekopa dinari mia tano, na mwingine hamsini.
42 Waliposhindwa kulipa madeni yao, huyo mtu aliwasamehe wote wawili. Sasa ni yupi kati ya hao wawili atampenda zaidi huyo bwana?”
43 Simoni akamjibu, “Ni dhahiri kwamba yule aliyesamehewa deni kubwa zaidi atampenda zaidi yule bwana.” Yesu akamwambia, “Sawa.”
44 Halafu akamgeukia yule mwanamke na kumwambia Simoni, “Unamwona huyu mwanamke, sivyo? Basi, mimi nilipoingia hapa nyumbani kwako hukunipa maji ya kunawa miguu yangu; lakini mwanamke huyu ameniosha miguu yangu kwa machozi yake na kunipangusa kwa nywele zake.
45 Wewe hukunisalimu kwa kunibusu, lakini huyu mwanamke tangu nilipoingia hapa amekuwa akiibusu miguu yangu.
46 Wewe hukunionyesha ukarimu wako kwa kunipaka mafuta kichwani, lakini huyu mwanamke amefanya hivyo kwa kunipaka mafuta miguu yangu.
47 Kwa hiyo nakwambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa ameonyesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehe kidogo, hupenda kidogo.”
Luka 7 in Biblia Takatifu

Luka 7:8-47 in Biblia ya Kiswahili

8 Kwani mimi pia ni mtu niliyewekwa kwenye mamlaka na nina askari chini yangu. Husema kwa huyu “Nenda” na huenda, na kwa mwingine, “Njoo” naye huja, na kwa mtumishi wangu 'Fanya hiki', na yeye hufanya”.
9 Yesu aliposikia haya alishangaa, na kuwageukia makutano waliokuwa wanamfuata na kusema.” Nawaambia, hata katika Israeli, sijawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama huyu.
10 Kisha wale waliokuwa wametumwa walirudi nyumbani na kumkuta mtumishi akiwa mzima.
11 fulani baada ya haya, ilitokea kuwa Yesu alikuwa anasafiri kwenda mji ulioitwa Naini. wanafunzi wake wakaenda pamoja naye wakiambana na umati wa watu.
12 Alipofika karibu na Lango la jiji tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake. aliyekuwa mjane, na umati wa wawakilishi kutoka kwenye jiji walikuwa pamoja naye.
13 Alipomwona, Bwana akamsogelea kwa huruma kubwa sana juu yake na akamwambia, “Usilie”.
14 Kisha akasogea mbele akaligusa jeneza ambalo walibebea mwili, na wale waliobeba wakasimama akasema “Kijana nasema amka”
15 Mfu akainuka na kukaa chini na akaanza kuongea. Kisha Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
16 Kisha hofu ikawajaa wote. wakaendelea kumtukuza Mungu wakisema “Nabii mkuu ameinuliwa miongoni mwetu” na “Mungu amewaangalia watu wake”
17 Hizi habari njema za Yesu zilienea Yudea yote na kwa mikoa yote ya jirani.
18 Wanafunzi wa Yohana walimwamwambia mambo haya yote.
19 Ndipo Yohana akawaita wawili wa wanafunzi wake na kuwatuma kwa Bwana kusema “Wewe ndiye yule ajaye, au kuna mtu mwingine tumtazamie?
20 Walipofika karibu na Yesu hawa wakasema, “Yohana mbatizaji ametutuma kwako kusema, 'Wewe ni yule ajaye au kuna mtu mwingine tumtazamie?”
21 kwa wakati huo aliowaponya watu wengi kutoka katika magonjwa na mateso, kutoka kwa roho wachafu, na kwa watu wenye upofu aliwapa kuona.
22 Yesu akajibu na kusema kwao. “Baada ya kuwa mmekwenda mlikotoka mtamjulisha Yohana mlichokiona na kukisikia. Wenye upofu wanapokea kuona na viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na kuwa hai tena, masikini wanaambiwa habari njema.
23 Na mtu ambaye hataacha kuniamini mimi kwa sababu ya matendo yangu amebarikiwa”.
24 Baada ya wale waliotumwa na Yohana kurudi walikotoka, Yesu akaanza kusema kwa makutano juu ya Yohana, “Mlikwenda nje kuona nini, mwanzi ukiwa unatikiswa na upepo?
25 lakini mlikwenda nje kuona nini, mtu aliyevaa vizuri? tazama watu wale wanaovaa mavazi ya kifalme na kuishi maisha ya starehe wako kwenye nafasi za wafalme.
26 lakini mnakwenda nje kuona nini, Nabii? Ndiyo, ninasema kwenu na zaidi sana kuliko nabii.
27 Huyu ndiye aliyeandikiwa, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya macho yenu, atakeyeandaa njia kwa ajili yangu,
28 Nasema kwenu, kati ya wale waliozaliwa na mwanamke, hakuna mkuu kama Yohana, lakini mtu asiye muhimu sana atakayeishi na Mungu mahali alipo yeye, atakuwa mkuu kuliko Yohana.”
29 Na watu wote waliposikia haya pamoja na watoza ushuru, walitangaza kuwa Mungu ni mwenye Haki. Walikuwepo kati yao wale waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
30 Lakini mafarisayo na wataalamu wa sheria za kiyahudi, ambao hawakubatizwa na yeye walikataa hekima za Mungu kwa ajili yao wenyewe.
31 Tena naweza kuwalinganisha na nini watu wa kizazi hiki? Wakoje hasai?
32 Wanafanana na watoto wanaocheza kwenye eneo la soko, wanaokaa na kuitana mmoja baada wa mwingine wakisema, 'Tumepuliza filimbi kwa ajili yenu, na hamkucheza. tumeomboleza na hamkulia.'
33 Yohana mbatizaji alikuja hakula mkate wala hakunywa divai, na mkasema “Ana pepo.
34 Mwana wa Mtu amekuja amekula na kunywa na mkasema, “Angali ni mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!
35 Lakini hekima imetambulika kuwa ina haki kwa watoto wake wote.”
36 Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale.
37 Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato.
38 Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato.
39 Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.
40 Yesu akajibu na kumwambia, “Simoni nina kitu cha kukuambia. “Akasema” “Kiseme tu mwalimu!”
41 Yesu akasema “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini.
42 Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi?
43 Simoni akamjibu na kusema, “Nadhani aliyesamehewa zaidi.” Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.”
44 Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, “Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake.
45 Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu.
46 Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato.
47 Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu.”
Luka 7 in Biblia ya Kiswahili